Featured Kitaifa

TPA YABAINISHA VIPAUMBELE VITANO KWENYE MPANGO MKAKATI WAKE WA NNE

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi wa Mipango,Ubora na udhibiti vihatarishi wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Dkt.Boniphace Nobeji,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Agosti 13,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo katika mwaka wa fedha 2022/23

…………………………………

Na Eva Godwin.DODOMA

IMEELEZWA kuwa Katika kipindi kilichoanzia mwezi Julai 2021 hadi Juni, 2022, hali ya utendaji wa Mamlaka ya usimamizi wa bandari TPA ilikuwa na Jumla ya Shehena iliyohudumiwa Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022, t b7ii iliyohudumiwa ni Tani milioni 20.665 sawa na ongezeko la asilimia 16 ya Tani bij – u- ù- – – – 17.775 milioni iiiìi.i ii mwaka (Julai 2020 hadi Juni 2021).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mipango,Ubora na Udhibiti Vihatarishi (kny:Mkurugenzi Mkuu TPA) Dkt. Boniphace S. NOBEJI alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na mwelekeo katika mwaka wa fedha 2022/23 Jijini Dodoma.

Amesema kuwa Shehena ya Makasha (Twenty Foot Equivalent Unit – TEUs)
Idadi ya Makasha yaliyohudumiwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022 ilifikia Makasha (TEUs) 823,404 sawa na ongezeko la asilimia 12 ya makasha (TEUs) 735,442 yaliyohudumiwa katika kipindi kama hiki mwaka uliopita (Julai 2020 hadi Juni 2021).

“Shehena ya Magari iliyohudumiwa katika Bandari ya Dar es Salaam kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022 ni 203,932 sawa na ongezeko la asilimia 38 ya magari 147,566 yaliyohudumiwa mwaka uliopita (Julai 2020 hadi Juni 2021)”, amesema

“Shehena ya Masoko ya Nchi Jirani
Shehena ya nchi jirani iiliyohudumiwa katika Bandari ya DSM katika kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022 ni Tani 7.801 milioni sawa na ongezeko la asilimia 39.9 ya Tani 5,580 milioni iliyohudumiwa mwaka (Julai 2020 hadi Juni 2021). Nchi jirani zinazohudumiwa na Bandari ya Dar es salaam ni DR-Congo, Zambia, Malawi, Rwanda, Burundi, Uganda, Zimbabwe, Comoro na Sudan Kusini”. Amesema Nobeji

Aidha amesema kuwa TPA imejiwekea Vipaumbele Vitano ambavyo viko kwenye Mpango Mkakati wake wa Nne (the TPA 4th Corporate Strategic Plan 2021/22-2025/26).

” Vipaumbele hivyo ni pamoja na Ujenzi wa Miundombinu ya Bandari Bora na yenye Mitambo ya Kisasa na sahihi ya Kuhudumia Meli na Shehena,Kuwa na Rasilimali Endelevu (Rasilimali watu na Rasllimali Fedha)”, amesema

“Matumizi ya Teknolojia za Kisasa kupitia Mifumo ya TEHAMA funganishi na aina za meli, shehena na pia mifumo ya kitaifa,Kuongeza Shehena ya nchi jirani inayohudumiwa na bandari za Tanzania na Kuimarisha masuala ya ulinzi, usalama na mazingira katika utoaji wa huduma pamoja na kuzingatia miongozo ya kimataifa iliyoridhiwa na nchi na Vipaumbele hivi vinatekelezwa na TPA kupitia Mipango na bajeti za kila mwaka”. Amesema Nobeji

Ameongezea kwa kusema Kutokana na Juhudi za Kuboresha Mazingira ya Ufanyaji Biashara na Kuvutia wa Wekezaji Nchini, zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Sekta ya Bandari imepata mafanikio makubwa Baadhi ya Mafanikio hayo kama ni Bandari ya Dar es Salaam ilipokea na kuhudumia Meli kubwa ya MV. GLAND DUKE PANAMA iliyoshusha Magari yapatayo 4,041 ikiwa ni idadi ya juu ya Magari kuwahi kuhudumiwa katika Bandari za Tanzania”, amesema

” Bandari ya Tanga imeweza kuhudumia meli kubwa za mafuta kama ifuatavyo, MT.UACC Sila iliyoshusha tani 39,811.762, Mv.NOD JOY iliyoshusha tani 36,448 na MV.SILVER ZOE iliyoshusha tani 38,446 sawa na jumla ya tani Tani 114,707 kwa meli zote tatu hivyo kuvunja record ya Tani za mafuta zilizowahi kuhudumiwa Bandari ya Tanga. Pia, Bandari ya Tanga imehudumia meli ya clinker ya Mv.Star Fighter iliyo beba tani 49,500 ikiwa shehena kubwa kwenda Rwanda kuwahi kuhudumiwa katika Bandari ya Tanga”. Amesema

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ilianzishwa kwa Sheria ya Bandari Namba 17 ya Mwaka 2004 kama ilivyorekebishwa mwaka 20

About the author

mzalendoeditor