Uncategorized

KINANA:’WANAODAI URAIS WA SAMIA NI WA KATIBA SIO WA KWELI’

Written by mzalendoeditor

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akipokea matembezi ya wana CCM ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, yaliyofanyika Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini, Iddi Ali Ame, wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, lililoandaliwa na CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja na kufanyika Mahonda,  Wilaya ya Kaskazini B, mkoani humo.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati akiwasili Afisi Kuu ya CCM, Mkoa wa Kaskani Unguja kulipofanyika kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, Wilaya ya Kaskazini B, mkoani humo.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akiwa na viongozi wengine wa Chama wakifuatilia kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, lililoandaliwa na CCM katika Mkoa huo na kufanyika Mahonda, Wilaya ya Kaskazini B, mkoani humo.

Vijana wakifuatilia kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, lililoandaliwa na CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja lililofanyika Mahonda, Wilaya ya Kaskazini B, mkoani humo. Katika kongamano hilo Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, alikuwa mgeni rasmi.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan lililoandaliwa na CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, na kufanyika Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja. Mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana  akizungumza wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan lililoandaliwa na CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, na kufanyika Mahonda Wilaya ya Kaskazini B.

About the author

mzalendoeditor