Featured Kitaifa

DAWASA YATAJA MIKAKATI KUMALIZA KERO YA MAJI DAR ES SALAAM

Written by mzalendoeditor

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja,akizungumza na waandishi wa habariĀ  leo Agosti 13,2022 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2022-2023.

………………………………………..

Na Eva Godwin-DODOMA

MAMLAKA ya Majisafi Na usafi wa Mazingira Dar-es-salaam(DAWASA) imefanikiwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za majisafi Kwa wakazi ndani ya eneo lake zaidi ya asilimia 96 kupitia utekelezaji wa Miradi mikubwa ya kimkakati na Miradi midogo ya kusogeza Mtandao wa Wananchi

Hayo yamesemwa leo Agosti 13,2022 jijini Dodoma na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja,wakati akizungumz na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2022-2023.

Amesema kuwa sehemu kubwa ya eneo linalohudumiwa Na Dawasa linapata huduma ya Maji ya uhakika baada ya miradi ya kimkakati kukamilishwa ikiwemo upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu Na Ruvu chini,ulazaji wa mabomba makubwa Na madogo na ujenzi wa matenki ya kuhifadhia maji

“Hii kupelekea idadi ya wateja kuongezeka kutoka wateja 217,766 mwaka 2018 hadi kufikia wateja 370,982 mwaka huu 2022.

“Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Dawasa inatekeleza miradi 13 ya majisafi Na usafi wa mazingira yenye thamani ya shilingi zipatazo Trilioni 1.029”, amesema

Aidha amesema Miradi mingi inatarajiwa kukamilika kabla ya Disemba 2022 hii ikiwa ni pamoja na mradi wa Maji kigamboni, mradi wa Maji Chalinze awamu ya tatu, mradi wa Maji Mshikamano, Mradi wa uboreshaji wa mfumo wa usambazaji Maji kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi hadi Bagamoyo na baadhi ya Miradi wa kusogeza huduma za Majisagi na usafi wa Mazingira katika maeneo yaliyo nje ya mtansao wa DAWASA.

Ameongezea kwakusema ilikuwa na vyanzo vya uhakika vya Maji katika eneo la huduma la DUWASA litakaloendana na ongezeko ya idadi ya Watu na Matumizi ya shughuli za maendeleo ikiwemo Viwanda, Miradi mikubwa miwili inatarajiwa kuanza kutekelezwa ndani ya Mwaka wa fedha 2022 hadi 2023.

“Miradi hii ni ya ujenzi wa bwawa la kidunda kuhakikisha Maji yanapatikana mwaka mzima katika mto Ruvu na ujenzi wa Mtambo mkubwa wa uzalishaji Maji katika Mto Rufiji”,amesema

“Mradi wa Rufiji unatarajiwa kuzalisha lita milioni 750 za Maji kwa siku na hivyo uzalishaji Maji utaongezeka mara dufu na hivyo kuwa na uhakika wa upatikanaji wa Maji ambayo ni Muhimu kwa Uhai na Maendeleo ya Kiuchumi”. Amesema Luhemeja

Katika kukamilika kwa utekelezaji wa Miradi hiyo ya Majisafi na usafi wa mazingira, Kazi itakayobaki itahusisha usogezaji wa huduma kwa Wananchi na kufanya maunganisho kwa Wateja Wapya.

About the author

mzalendoeditor