Na Eva Godwin- Dodoma
WIZARA ya Kilimo imeongeza bajeti ya utafiti na uzalishaji wa mbegu za awali kutoka Shilingi Bilioni 11.63 kwa mwaka 2021/2022 hadi Shilingi Bilioni 40.73 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la asilimia 250.
Hayo yamezungumzwa leo Agosti 11, 2022 na Na msimamizi wa menejimenti ya maarifa na mawasiliano ya umma kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania Dkt Richard Kasuga wakati akizungumza Na waandishi wa habari akielezea utekelezaji wa shughuli za taasisi Na mwelekeo wa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023.
Amesema kuwa Bajeti hiyo, itatumika kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora kwa kuongeza uzalishaji wa mbegu za awali za mazao ya nafaka, mikunde na mbegu za mafuta kutoka tani 226.5 hadi tani 1,453 ambazo zitakidhi mahitaji ya Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) na kampuni binafsi.
” TARI imepanga kuzalisha teknolojia mpya zikiwemo aina za mbegu zenye sifa zaidi ya zile zinazotumiwa kwa sasa, aina hizo za mbegu zina sifa ya kutoa mavuno mengi, kustahimili ukame, ukinzani dhidi ya magonjwa na wadudu, zenye viinilishe vingi, pamoja na sifa zingine za soko kama vile sifa za mezani na Teknolojia zingine zitakazogunduliwa ni za uongezaji thamani katika mnyororo wa thamani wa mazao pia kuboresha afya ya udongo; kugundua mbinu bora za ukuzaji mazao, zana bora za kilimo, na utunzaji wa mazao baada ya mavuno pamoja na kuimarisha uchumi jamii”,
amesema
“TARI imetengewa jumla ya shilingi bilioni 54,108,361,807 Kati ya fedha hizo shilingi 12,977,566,054 ni fedha za mishahara (24%), shilingi 1,928,325,000 fedha za matumizi mengineyo (4%) na shilingi 39,202,470,753 ni za maendeleo (72%)”.Amesema Kasuga
Ameongezea kwakusema miche na pingili zipatazo milioni 50 ya mazao mbalimbali ambayo ni parachichi, mkonge, michikichi, minazi, mihogo, viazi vitamu na ndizi itazalishwa na kusambazwa kwa wakulima.
“Aina 141 za mbegu za asili zitasafishwa na kuhifadhiwa katika vituo vya TARI kwa ajili ya kuzifanyia utafiti na kuziboresha ,Utafiti wa mbegu za asili utaongeza wigo katika kukidhi mahitaji ya soko na kilimo cha biashara kwa kushirikiana na viwanda pamoja na wafanyabiashara”,amesema
“Ghala tano (5) yenye uwezo wa kuhifadhi tani 415 za mbegu kila moja yatajengwa katika vituo vya TARI Makutupora, TARI Seliani, TARI Hombolo, TARI Kifyulilo na TARI Dakawa,Ujenzi huo ukikamilika utaongeza uwezo wa kuhifadhi mbegu kutoka tani 20 za sasa hadi tani 2,075 kwa vituo hivyo na Vilevile, ghala tano za kuhifadhi mbegu zitakarabatiwa katika vituo vya TARI Uyole (3) na TARI Ilonga (2)”.Amesema Kasuga