Featured Kitaifa

MAKADA 178 WA CCM WACHUKUA NA KUREJESHA FOMU KUWANIA UBUNGE WA EALA 

Written by mzalendoeditor

 

Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni, Dk Costico Maudline,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Agosti 10,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya kufungwa kwa dirisha la kuchukua na kurejesha fomu kuwania nafasi ya kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.

………………..

Na Alex Sonna-DODOMA
MAKADA 24 wa CCM wamejitokeza kuchukua na kurejesha  fomu siku ya mwisho ya kufungwa dirisha na kufanya idadi ya wagombea wa nafasi tisa za ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kufikia 178.
Akizungumza baada ya kufunga dirisha la uchukuaji fomu kuwania nafasi za ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni, Dk Costico Maudline
, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ,amewapongeza wagombea wote waliochukua na kurudisha fomu hizo.
“Wamefanya uamuzi wa kishujaa wa kutimiza wajibu wao wa kikatiba wa wanachama wa CCM wa kuchaguliwa au kuchagua” amesema Dk.Maudline
Maudline amesema kuwa, baada ya kufungwa dirisha hilo wagombea wote wawe na subira, waendelee na shughuli zao za kila siku za kujenga taifa hadi pale taarifa nyingine itakapotolewa na CCM.
Aidha amesema kwa idadi hiyo ya wagombea waliojitokeza kuchukua fomu na kurejesha bila kukosa ni ishara tosha kwamba CCM ndicho chama pekee kinachojali na kuzingatia haki na wajibu wa wanachama wake katika dhima ya demokrasia.
Amesema dirisha hilo lililotangazwa Julai 28, mwaka huu na kuanza uchukuaji Agosti mosi limefungwa rasmi saa 10.00 jioni Agosti 10, mwaka huu.
Kabla ya jana, jumla ya makada 155 walikuwa wamechukua fomu katika Afisi Kuu za CCM Zanzibar, Ofisi Ndogo za CCM Lumumba, Dar es Salaam na Ofisi Kuu Dodoma ambazo kila kada alitakiwa kulipia Sh milioni moja kabla ya kupewa na kujaza fomu hiyo.
Waliochukua fomu  katika siku ya mwisho ya kufunga dirisha katika ofisi kuu Dodoma ni pamoja na aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige.
Wengine waliochukua katika makao makuu ya CCM Dodoma ni Dk Ally Nkwabi, Zabron Zaphania Wakalo, Clion Odhiambo Dismas, Leonard Mandago Masai na Edna Peter Chandeu.
Pia ni Josephelias Sabuka, Martin Lissu, Fadhili Rajabu Maganya, Frank Mathew Machui, Dk Wemael Allen Chamshama na Mshinwa Edith Banzi.
Waliochukua fomu ofisi ndogo za Lumumba Dar es Salaam ni Mshindi Andrew Lwamhulu, Dk Leonard Subi, Imelda Isack Mwamanga, Lusubilo Joel Mwakabibi, Jalia Abbakari Mayanja, Ussy Brighton Charugamba na Ally Kassim Mandai.
Wengine ni Zena Athumani Simkondo, Edward John Nyerere, Gwakisa George Makaranga, Gidion Kaino Mandesi na Janice Benson Kimaro. Hakuna aliyechukua fomu Afisi kuu Zanzibar hakuna aliyechukua fomu.

About the author

mzalendoeditor