Featured Kitaifa

WAKULIMA WAENDELEA KUNUFAIKA NA KILIMO KWA MFUMO WA KIDIGITALI

Written by mzalendoeditor

Baadhi ya bidhaa za Mezzanine zikiwa katika banda la maonyesho ya nanenane leo Agosti 9,2022 Jijini Dodoma

Baadhi ya Watu wakipata maelekezo kwenye banda la maonyesho ya nanenane kutoka kwa wataalamu wa kampuni ya Mezzanine Leo Agosti 9,2022 Jijini Dodoma

……………………………………..

Na Eva Godwin-DODOMA

KAMPUNI ya Kilimo ya Mezzanine iliyopo Mkoani Singida imefanya mabadiliko ya kidigitali CONNECTED FARMER kwenye mfumo wa kilimo biashara ambapo inamuunganisha mkulima kupata pembejeo kwa bei nafuu

Hayo yamezungumzwa na Maria Sito ambae ni Mfanyakazi kutoka Mezzanine Leo Agosti 9, 2022 Jijini Dodoma katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati ikiwa ni maonyesho ya 28.

Amesema wamelazimika kutumia mfumo huo kutokana na Watu wengi kuwa na mtazamo hasi kuwa kilimo ni kitu kisicho na tija hivyo wamelazimika kuja na mfumo huo unaowashawishi wengi kulima kibiashara.

” Mbegu zetu zinavumilia ukame na Mfumo huu wa kidigitali unamsaidia mkulima akijiunga kwenye mfumo anapata faida kutokana na kupata pembejeo bora pamoja na soko la uhakika ikiwa ni tofauti na madalali”,amesema

” Tunampunguzia gharama Mkulima na akihitaji pembejeo anaweza kupata pembejeo kwa bei nafuu na malipo yake analipa kwa njia ya simu na taarifa zake tunaziona kwa njia hiyo ya simu, na Wakulima wengi tumeona wameufurahia huu mfumo”.Amesema Sito

Naye Geogre Makala ambaye pia ni mfanyakazi wa Kampuni hiyo amesema kuwa huwa wana utaratibu wa kumwezesha mkulima kwa kumpatia mbegu na mbolea ambapo mkulima atatoa asilimia 20% na Mkulima atakapovuna atarudisha 80% huku akiwa chini ya Maafisa ugani wanaokuwa nae sambamba kuanzia hatua ya kulima hadi kufikia uvunaji wa mazao yake.

” Lakini hapo atakuwa chini ya Maafisa ugani ambapo pia watakuwa wanatembelea shamba lako na kumuelekeza jinsi ya upandaji na upalilizi wa kisasa

“Kwaio yeye Mkulima hawezi kupata hasara kutokana na kusimamiwa na wataalamu ambao kampuni yetu ndio itawalipa na pia tunamtafutia soko la kuuza bidhaa yake pale ambapo atavuna zao lake”.Amesema Makala

Ameongezea kwa kusema kuwa Kampuni hiyo imelenga kumuinua Mkulima mdogo kulima kibiashara ikiwa itamtafutia soko la mazao ambayo yatakuwa na bei mara mbili tofauti na bei za sokoni kutokana na mkulima huyo kujiunga na kampuni ya Mezzanine.

About the author

mzalendoeditor