Featured Michezo

OKWA ATUMA SALAMU JANGWANI,YAFUNIKA SIMBA DAY

Written by mzalendoeditor
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
 
SIMBA DAY, wanamsimbazi leo ni kama ilikuwa siku yao mara baada ya kupokea burudani mbalimbali kutoka kwa wasani, viongozi wao pamoja na wachezaji wao ambao wamezesha mashabiki kumaliza siku ya leo wakiwa na furaha.
 
Kwanza kabisa mashabiki waliamuakuujaza uwanja wa Benjamini Mkapa ili kuweza kushuhudia burudani kadhaa zikitolewa kwenye uwanja huo.
 
Wasanii kibao wameweza kutoa burudani mbalimbali kama Zuchu, Tunda Man na wengine kibao ambao wametoa burudani ambayo mashabiki walizipokea kwa shangwe kwenye dimba hilo.
 
Nje ya burudani hizo kulikuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya St.George ya nchini Misri na kuwafanya Simba Sc kutoka kifua mbele kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
 
Wachezaji wapya ambao wametambulishwa leo hii wameonesha viwango ambavyo mashabiki walitarajia, wachezaji hao ni kama Nelson Okwa ambaye alifunga kwenye mchezo huo,

About the author

mzalendoeditor