Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYA RUNGWE NA KYELA

Written by mzalendoeditor

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Kyela kwenye  Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale Wilayani Kyela Mkoani Mbeya .

………………………..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema mkoa wa Mbeya unakabiliwa na changamoto ya lishe bora kwa watoto licha ya kuwa mkoa huo unalima na kuzalisha chakula kwa wingi. 

Rais Samia amesema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa John Mwakangale wilayani Kyela.

Aidha, Rais Samia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuhakikisha anatekeleza Mpango wa Pili Jumuishi wa Kitaifa wa Masuala ya Lishe (NMNAP II 2021 – 2026).

Vile vile, Rais Samia amewataka wananchi wa mkoa huo kuongeza jitihada katika masuala ya lishe bora ili kuimarisha afya za watoto.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuwa na umoja na mshikamano na kufanya kazi kwa kushirikiana bila ya kujali itikadi zao.

Rais Samia ameendelea na ziara yake mkoani Mbeya ambapo leo ametembelea Wilaya ya Rungwe na Kyela na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuweka jiwe la msingi ujenzi wa kituo cha pamoja cha forodha mpakani mwa Tanzania na Malawi.

About the author

mzalendoeditor