Featured Kitaifa

WAZIRI NDAKI ATAKA WAFUGAJI KUZALISHA KWA TIJA

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu ‘Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo”yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni  kanda ya kati Jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Staki Senyamule,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu ‘Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo”yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni  kanda ya kati Jijini Dodoma.

………………………………….

Na Eva Godwin-DODOMA

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amevitaka vyuo Vikuu na Taasisi za utafiti kupeleka Teknolojia wanazozifanya kwa wananchi ili wapate maarifa na namna ya kufuga na kuzalisha kwa Tija kwa maslahi ya Taifa na Watu wake.

Amezungumza hayo Leo Agosti 5,2022 wakati akizindua Maonyesho ya sikukuu ya Wakulima na Wafugaji kanda ya kati Jijini Dodoma.

Ndaki amesema kutoka mwaka 2023 hadi 2027 Serikali imepanga kuleta Mabadiliko makubwa katika sekta ya Mifugo kwa kuwaelimisha wafugaji kufuga kibiashara kwa kuwapatia elimu ya kuwa na mbegu bora za Mifugo ya kisasa huku akisisitiza ubora wa bidhaa ni muhimu sana ili kushindanisha katika soko la ndani na Nje ya nchi.

“Kumekuwa na Taasisi nyingi ambazo zinausika na kutoa elimu juu ya mbegu bora za ufugaji ambao unaweza kukuingizia kipato kikubwa”,amesema

“na kikubwa zaidi mzingatie ubora wa bidhaa ambazo mnanunua na kuuza ili pia muweze kushindanisha katika masoko makubwa yaliyopo Ndani na Nje ya Nchi”.Amesema Ndaki

Ameongezea kwa kuzitaka Almashauri kote nchini kuhakikisha wanashirikiana na watoa huduma kuweka hereni mifugo yote mpaka ifikapo tarehe 30 septemba mwaka huu zoezi hilo liwe limekamilika.

“Zoezi hili nimmuhimu sana inaraisisha kufuga mifugo kibiashara na inaongeza thamani ya mifugo yetu

“zoezi hili litapunguza unyang’anyi na uwizi wa mifugo yetu kwaio naomba kuanzia almashauri zote za mikoa mzingatie hili suala mpaka ifikapo tarehe 30 Septemba muwe mmeshakamilisha zoezi hili”.Amesema Ndaki

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema Dodoma ndio makao makuu ya Serikali hivyo wafugaji na wakulima wanaotakiwa kulima na kufuga kisasa licha ya dodoma kuwa na machinjio ya kisasa bado kumekuwa na changamoto ya mifugo michache inayochinjwa katika machinjio hiyo ya kisasa iliyoko kizota.

“Tunayo eneo kubwa sana la kisasa na eneo hili linakadiriwa kuwa ni ekta milioni Moja (1) na Laki Mbili (2) ambayo ni kama 29%ya Mkoa mzima wa Dodoma, kwaio ukiona eneo hili ni kubwa la kufugia”,amesema

“Na kwa Mkoa wa Dodoma tuna sifa zote za kufuga kwa maana ya eneo na kwa maana ya idadi ya kufuga na Kazi tuliyokuwa nayo nikuongeza tija katika ufugaji wa kisasa”.Amesema Senyamule

Aidha Dkt. Charles Mhina kwa niaba ya katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi amesema kutoka mwaka 2023 hadi 2027 Serikali imepanga kuleta Mabadiliko makubwa katika sekta ya Mifugo kwa kuwaelimisha wafugaji kufuga kibiashara kwa kuwapatia elimu ya kuwa na mbegu bora za Mifugo ya kisasa ili kumfanya Mfugaji akue kisasa na kuwa na mifugo yenye tija.

About the author

mzalendoeditor