Featured Michezo

VIPERS YATIA DOA SIKU YA MWANANCHI

Written by mzalendoeditor

MABINGWA wa Ligi Kuu ya Uganda VipersĀ  SC wametia Doa Siku ya Mwananchi baada ya kuwachapa Mabingwa wa Ligi ya NBC Tanzania bara Yanga mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Vipers walipata bao la kwanza kabisa dakika ya 1 baada ya wachezaji kujichanganya na Mshambuliaji Milton Karisa akipiga bao la kwanza bao lilidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko na kuwaingiza wachezaji wake wapya waliosajiliwa msimu huu wakiongozwa na Aziz Ki Stepher,Bernard Morrison,Joyce Lomalisa,Gael Bigirimana.

Hata hivyo mabadiliko hayo hayawakuwasaidia mnamo dakika ya 64 Anukani Bright alifunga bao la pili kwa mpira wa Kona ulioenda moja kwa moja.

Yanga wanarudi tena kambini kujianda na mechi ya ngao ya jamii dhidi ya watani wao wa jadi Simba mchezo wa ufunguzi wa Ligi utakaopigwa Agosti 13,2022

About the author

mzalendoeditor