Kitaifa

TRC KUONGEZA UFANISI WA UTENDAJI KAZI KWA KUBORESHA ZAIDI MIUNDOMBINU NCHINI

Written by mzalendoeditor

 

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika  la Reli Nchini (TRC) Masanja Kadogosa,akizungumza   na waandishi wa habari leo Agosti 6,2022 jijini Dodoma kuhusu shughuli za TRC na Vipaumbele vipaumbele vya taasisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2022/23. 

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika  la Reli Nchini (TRC) Masanja Kadogosa,akielezea mikakati ya TRC wakakati akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 6,2022 jijini Dodoma kuhusu shughuli za TRC na Vipaumbele vipaumbele vya taasisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2022/23. 

WAANDISHI wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika  la Reli Nchini (TRC) Masanja Kadogosa,wakati akizungumza  leo Agosti 6,2022 jijini Dodoma kuhusu shughuli za TRC na Vipaumbele vipaumbele vya taasisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2022/23. 

…………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika  la Reli Nchini (TRC) Masanja Kadogosa,amesema kuwa mwaka wa fedha 2021/22_2022/23  wamejikita zaidi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi ya shirika Kwa kujenga,kukarabati na kuboreshwa miundombinu ya Reli.

Kadogosa ameyasema hayo leo Agosti 6,2022 jijini Dodoma wakati akitoka taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya shirika hilo kwa mwaka 2021/22.

Kadogosa amesema shirika hilo limejipanga kutekeleza mipango ya kitaifa katika uboreshaji na uendelezaji wa miundombinu ili kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kukuza biashara ndani na nje ya Nchi.

“Ili kufikia adhima ya ufanisi,shirika litahakikisha linaboresha miundombinu ya Reli Kwa kujenga mtandao mpya wa Reli wa kiwango Cha standard Gauge wenye jumla kilimeta 4,777 na ukarabati mtandao wa Reli iliyopo ya Meter Gauge Kwa kilimeta 2537,”amesema Kadogosa

Amesema, ukarabati huo wa njia ambao utajumuisha kuinua uwezo wa njia Kwa kuondoa reli nyepesi za paundi 45na 56 na kutandika Reli nzito za paundi 80,kuinua uwezo wa madaraja kutoka ekseli 13.5 kufikia ekseli 18.5 pamoja na kuboreshwa mfumo wa ishara na mawasiliano.

Amesema shirika hilo linatekeleza miradi ya muda mfupi, muda wa kati na mrefu ,pia muda mfupi inajumuisha miradi ufufuaji wa njia za zamani ikiwemo njia ya kaskazini ,miradi ya muda wa kati inajumuisha ukarabati wa njia iliyopo ikiwemo uboreshaji wa njia ya kati ambao umefanyika kupitia Mradi wa Tanzania Intermodal and tall Development project (TIRP) kutoka Dar es salaam hadi Isaka, Miradi ya muda mrefu ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR).

“Serikali inajenga mfumo wa umeme wa msongo wa kilovoti 220 ambao unajitegemea (dedicated line) kwa ajili ya uendeshaji wa treni ili kupata umeme wa uhakika,Kwa kipande Cha Dar es salaam mpaka Morogoro mfumo huo una urefu wa kilimeta 160 na umekamilika Kwa asilimia100,mkandarasi ameshalipwa kiasi Cha bilioni 70.6,”amesema.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari maelezo Gerson Msigwa,amesema kuwa  ujenzi wa reli hiyo unaenda sambamba na Maboresho ya bandari zilizopo nchini kwa kuwa miundombinu hiyo ni mahsusi kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo mizito.

About the author

mzalendoeditor