Featured Kitaifa

TBS YATAKATA MAONESHO YA NANENANE JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

 

MENEJA wa kanda ya kati wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Nickonia Mwabuka, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la shirika hilo katika Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu ‘Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo”yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni  kanda ya kati Jijini Dodoma.

MENEJA wa kanda ya kati wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Nickonia Mwabuka,akimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda hilo ili kupata elimu zaidi kuhusu ubora wa bidhaa katika Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu ‘Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo”yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni  kanda ya kati Jijini Dodoma.

MKAGUZI wa TBS Kanda ya Kati,Magesa Mwizarubi,akitoa elimu kwa wananchi pamoja na wanafunzi waliofika katika banda la TBS wakati wa Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu ‘Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo”yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni  kanda ya kati Jijini Dodoma.

……………………………

Na Alex Sonna _DODOMA 
 
SHIRIKA  la Viwango Tanzania (TBS) limewakumbusha wajasiriamali wakubwa na wadogo kuhakiki ubora wa bidhaa zao pamoja na  kuhakikisha wanaweka vifungashio vyenye ubora ili kuvutia sokoni.

Pia imewakumbuisha kutengeneza bidhaa ambazo zinakidhi soko la kitaifa na kimataifa.

Hayo yameelezwa leo Agosti 6 ,2022 mwaka huu na Meneja wa kanda ya kati wa shirika hilo,Nickonia Mwabuka wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la shirika hilo lililopo  nane nane Nzuguni Jijini Dodoma.

TBS ipo katika maonesho hayo na imekuwa ikitoa elimu kwa watanzania kuhusu kazi zinazofanywa na shirika hilo ikiwemo ile ya kuhakikisha kuwa bidhaa zote zinazoingia Tanzania zinakidhi usalama wa afya.

Mwabuka amesema  wajasiriamali wakubwa na wadogo wana wajibu wa kuhakikisha wanaweka vifungashio vyenye ubora ili kuvutia sokoni na ndani na nje ya Tanzania.

“Kama tutakuwa na bidhaa ambazo ni hafifu soko letu la Tanzania litavamiwa tunawasihi na kuwakumbusha wajasariamali waje wahakiki ubora wa bidhaa zao.

Amesema katika banda lao wanatoa elimu kwa wajasiriamali lengo likiwa ni kuhakikisha wanatoa bidhaa zenye ubora na zenye mahitaji ya soko husika.

“Kilimo ni biashara, kwenye biashara ni lazima uwe na biashara zinazokidhi viwango vya ndani na nje ya nchi.Kumbuka kwamba Tanzania ni wanachama  wa Jumuiya ya  Afrika Mashariki na pia ipo SADC   mahitaji ni makubwa bidhaa lazima zikidhi vigezo,”amesema Meneja huyo wa Kanda.

Katika hatua nyingine,Meneja huyo amesema TBS imetenga zaidi ya Shilingi bilioni 250 kwa ajili ya kutoa elimu kwa wajasirimali kuhusu umuhimu wa kutengeneza bidhaa zenye ubora.

“Lakini pia wajasiriamali wakubwa nao pia tunawapa  elimu ya ubora lakini kubwa ambalo tunazingatia ni suala la vifungashio katika bidhaa zetu.

“Na Waziri wa Mifugo na Uvuvi alizungumzia kwa undani lazima vifungashio  vikidhi vigezo na soko letu litakuwa halina ushindani,”amesema meneja huyo.

Hata hivyo amewataka waandishi wa habari kuendelea kuwakumbusha watanzania kutengeneza bidhaa zenye kukidhi matakwa ya viwango ili waweze kushindana ndani na nje ya nchi.

About the author

mzalendoeditor