Featured Kitaifa

SPIKA DKT.TULIA APONGEZA JITIHADA ZA BENKI YA NBC KUINUA SEKTA YA KILIMO

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (kushoto) akielezea kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson (katikati) huduma mbalimbali mahususi kwa wakulima zinazotolewa na benki hiyo wakati alipotembelea banda  la benki hiyo kwenye Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (kushoto) akimuelezea Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson (wa tatu kulia) kuhusu huduma mbalimbali mahususi kwa wakulima zinazotolewa na benki hiyo wakati alipotembelea banda la benki hiyo kwenye Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.

Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbeya Bi Asia Mselemu (kushoto) akimuelezea Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson (kulia) kuhusu huduma mbalimbali mahususi kwa wakulima zinazotolewa na benki hiyo wakati alipotembelea banda  la benki hiyo kwenye Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya. Wanaomsikiliza ni pamoja na Mkuu wa wilaya ya Songwe Simon Simalenga (Katikati)

…………………………………..

Na Mwandishi Wetu-Mbeya

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson ameguswa na kupongeza jitihada za Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) katika kuboresha sekta ya kilimo hapa nchini kupitia huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa wadau wa sekta hiyo muhimu.

Akizungumza wakati alipotembelea banda  la benki hiyo kwenye Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya, Dkt Tulia alionyesha kuvutiwa zaidi na huduma ya Bima ya Kilimo inayotolewa na benki hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance ikilenga kuwalinda wakulima, wavuvi na wafugaji nchini dhidi ya hasara pindi wanapopata majanga mbalimbali yanayoweza kuathiri uzalishaji wao.

“Pamoja na huduma zote nzuri mnazozitoa benki ya NBC kwa wakulima nimevutiwa sana na huduma ya Bima ya kilimo kwa wakulima. Nimevutiwa zaidi  baada ya kusikia tayari kuna wakulima wa tumbaku huko mkoani Tabora wameshanufaika na huduma hii. Hiki ni kithibitisho tosha kuwa huduma hii inatekelezeka vizuri kwa faida ya wakulima wetu…hongereni sana kwa kuonesha njia,’’ alipongeza.

Mbali na huduma hiyo, akiwa kwenye banda la benki hiyo Dkt Tulia alipata wasaa wa kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kupitia mkakati mkubwa wa benki hiyo unaolenga kuinua sekta ya kilimo nchini unaofahamika kama ‘NBC Shambani’ unaohusisha mnyororo wote wa sekta ya kilimo kuanzia kwa mkulima, mchakataji wa mazao ya kilimo hadi msambazaji.

“Kupitia mpango wetu wa NBC Shambani tumekuwa tukishirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa mikopo mbalimbali kwa wakulima ikiwemo ya zana mbalimbali za kilimo ikiwemo matrekta na mashine nyingine nyingi,’’ alisema Bw Raymond Urassa, Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC wakati akielezea huduma hizo kwa Dkt Tulia.

Zaidi, Bw Urassa aliongeza kuwa benki hiyo pia inawawezesha wakulima kwa kuwapatia pembejeo za kilimo kwenye baadhi ya mazao hususani yale ya kimkakati ikiwemo pamba, kahawa na tumbaku lengo likiwa ni kuongeza tija kwenye sekta hiyo muhimu.

“Hivyo ninaomba sana wadau mbalimbali wa kilimo waliohudhuria maonesho hayo kutembelea banda letu la NBC ili kupata ufafanuzi na huduma mbalimbali zinazohusiana na sekta hii muhimu,’’ alisema.

About the author

mzalendoeditor