Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI WAWILI

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya teuzi zifuatazo:-

  1. Amemteua Bwana Eric Benedict Hamissi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL). Kabla ya uteuzi huo Bw. Hamissi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

  1. Amemteua Bw. Stephen Nzohabonayo Kagaigai kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).  Bwana Kagaigai anachukua nafasi ya Balozi Herbert E. Mrango ambaye amemaliza kipindi chake.

Teuzi hizi zinaanza mara moja.

About the author

mzalendoeditor