Featured Michezo

YANGA KUCHEZA NA MABINGWA WA UGANDA WIKI YA MWANANCHI

Written by mzalendoeditor
KLABU ya Yanga itashuka dimbani kuvaana na Mabingwa wa Ligi ya Uganda  Vipers kwenye kilele cha Siku ya Wananchi ambayo inatarajia kuwa Agosti 6 Mwaka huu.
Katika hatua nyingine Yanga wametoa ratiba ya shughuli mbalimbali ambazo watazifanya ndani ya siku tano kuelekea kwenye kilele cha  siku hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Makamu wa rais wa klabu hiyo na  Mwenyekiti wa kamati ya maaandalizi wiki ya wananchi Arafat Haji, alisema kwamba wamezindua rasmi jana maandalizi ya siku ya wananchi ambayo yataadhimishwa Agosti 6.
Alisema ratiba yao ya ana nikuzindua rasmi uwepo wa siku ya wananchi ambao umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel iliyopo jijini Dar es Salaam  na kesho watakuwa  Jangwani Sekondari kutoa msaada wenye lengo la kurudisha katika jamii.
Katika hatua nyingi Mwenyekiti wakamati alisema kesho jumatano watakuwa nambio zapamoja baina yao na washirika wao CRDB kutoka kwenye makao makuu yao hadi makao makuu ya klabu Jangwani.
“Alhamis tutakuwa natukio lakuchangia damu ambapo hilo tutashirikiana na wadhamini wetu wakuu Sport Pesa katika hospitali yataifa ya Muhimbili na ijumaa tutaanza kupokea wageni wetu ambao tumewaalika kutoka katika mataifa mbalimbali, ” alisema
Aidha  kamati hiyo ilitaja wasanii mbalimbali ambao watatumbuiza kwenye siku hiyo akiwemo Marioo, Stamina, Mzee wa Bwax na wengine wengi ambao wanafanya vizuri ndani nahata nje ya mipaka ya Tanzania.
” Tunakaribisha makampuni mengine kuja kuwekeza katika klabu yetu ya simba kama ambavyo wamefanya Mbet lakini pia nawakaribisha watu wote katika Simba Day Agosti 8, ” alisema

About the author

mzalendoeditor