Na Eva Godwin-DODOMA
MHANDISI wa Wizara ya habari, Mawasliliano na Teknolojia ya habari na mratibu wa utekelezaji wa Anwani za makazi, Jampioni Mbugi amewaomba Wananchi kutumia muda huu kuhakiki anwani zao za makazi kwa kujua namba zao za nyumba pamoja na majina ya barabara.
Ameyasema hayo leo Julai 29,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi la kuhakiki anwani za makazi Jijini Dodoma.
Amesema ni lazima kila anayekuja kuhakiki nilazima ajue jina la barabar,jina la kitongoji namba ya nyumba na vitu muhimu vinavyohitajika.
“Tukiwa tupo kwenye maandalizi hayo ya Sensa na makazi tunaomba Wananchi wote wajitokeze kuhakiki anwani zao za makazi kwa kujua namba yako ya nyumba , kujua jina la barabara inayopita mbele ya nyumba zenu pamoja na jina la kitongozi”,amesema
“hili zoezi litakamilika tarehe 10 Agosti, 2022 ili tuendelee na mipango mizima ya zoezi la Sensa na namna ya kujipanga kuhesabiwa”.Amesema Mbugi
Ameongezea kwakusema zoezi hili la kuandikisha anwani za makazi lilianza mwezi wa sita na muitikio wa Wananchi ni mzuri kutikana na Wananchi kujitokeza katika Serikali zao za mitaa,Vijiji na Vitongoji.
“Muitikio wa Wananchi ni mzuri sana kutokana na Wananchi wengi wamejitokeza kutoka sehemu mbalimbali za mitaa,vijiji na vitongoji vyao kujiridhisha taarifa zake za anwani
“Lakini pia Wananchi wengine wameenda mbali zaidi kupitia kwenye mfumo wa kidigitali ambao tunaita mfumo wa namba kuahakiki Anwani zao za makazi”.Amesema Mbugi
Naye Mtaalamu wa Mfumo wa Anwani za Makazi Jannet Peter amesema muitikio wa Wananchi katika suala la kuhakiki anwani za makazi ni mkubwa japo kuna changamoto nyingi ambazo zinajitokeza
“Wananchi wengi wanahamasika kuja kujua anwani zao lakini pia nilazima mtu ajue almashauri anapotoka kwasababu kumekuwa na changamoto nyingi katika kuwandikisha kuhakiki
“Mwingine anaweza kuja hajui Jina la barabara yake ,hajui namba ya nyumba yake wala kitongoji anapotoka na mwingine hata mwenyekiti wake hamjui hili”.Amesema Peter
Naye Moja kati ya Mwananchi ambae amefanya zoezi hilo la kuhakiki ,John Samson anayeishi kata ya Makulu ameelezea namna alivyohakiki amesema amelifurahia zoezi hili hivyo wananchi wajitokeze katika zoezi hili huku wakisubiri kuhesabiwa Agosti 23,2022
“Mara ya kwanza nilijihakiki nyumbani walipita lakini nikaona haitoshi ikabidi na leo hii pia nije nihakiki na zoezi hili nimelifurahia sana
” Kwasababu mimi nina nyumba pia Dar es salaam na pia hapa Dodoma lakini taarifa zangu zote nimezikuta zipo sahihi”.Amesema Samson