Featured Kitaifa

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA DHARURA WA BARAZA LA MAWAZIRI WA NCHI ZINAZOZALISHA ALMASI AFRIKA.

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Madini Dkt Dotto Biteko akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha kuhusiana na mkutano wa tatu wa dharura wa baraza la mawaziri wa nchi zinazozalisha Almasi Afrika unatarajiwa kufanyika kesho mkoani humo.

BAADHI ya waandishi wa habari mkoani Arusha wakiwa katika mkutano wao na waziri wa madini Dkt Dotto Biteko.

……………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Nchi 18 za Afrika zinatarajiwa kukutana kesho Julai 29,2022 katika Mkutano wa baraza la mawaziri kutoka nchi za Afrika zinazozalisha Almasi  lengo likiwa ni  kuidhinisha nyaraka muhimu za baraza hilo zilizofanyiwa marekebisho ikiwemo Katiba.
Akiongea na na waandishi wa habari juu ya mkutano huo waziri wa madini Dkt Dotto Biteko ambaye ni Mwenyekiti wa baraza hilo alisema kuwa katika mkutano huo mkutano huo nchi  18 zitashiriki huku 12 zikiwa ni wanachama  wanachama na sita ni waangalizi.
Alieleza kuwa wanachama ni nchi zinazozalisha Almasi ambazo zimefuata sheria za ADPA za sasa ambapo Tanzania ni mojawapo ikiwa nchi waangalizi ni zile ambazo jiolojia ina uwezo wa kuzalisha Almasi na mwisho zinaweza kuwa wazalishaji wa Almasi.
Alifafanua kuwa  nyaraka nyingine muhimu zitakazo idhinishwa ni kanuni na na miongozo ya umoja huo, pamoja na kuteua viongozi watatu wa sekretarieti ambao ni katibu mtendaji na manaibu wake wawili ambapo lengo la kuanzishwa kwa umoja huo ni kuzipatia nchi zinazalisha Almasi  Afrika jukwaa la kuzikutanisha katika kusudi moja.
“Lengo hilo ni ili kuhakikisha rasilimali ya madini hayo zinanufaisha nchi wanachama na katika kukutana huku nchi hizi zinashurikisha uzoefu na ushirikiano katika nyanja za anuai za sekta ya Almasi,” Alieleza Dkt Biteko.
Alieleza kuwa Tanzania kama wenyeji wa mkutano huo wameweza kujifunza zaidi kuhusu usimamizi wa sekta hususani kwa madini ya Almasi ambapo nchi wanachama na wasio wanachama walipata nafasi ya kujifunza kwao kuhusu namna walivyofanikiwa kuwaendeleza wachimbaji wadogo wakiwemo wa madini ya Almasi na madini ya dhahabu.
Hata hivyo nchi hizo ni pamoja na Angola, Botswana,Cameroon,Jamuhuri ya Afrika ya kati,Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo,Ghana,Guinea,Namibia ,Sierra Leone, South Africa, Tanzania, Togo, na Zimbabwe ikiwa nchi waangalizi ni Algeria, Jamuhuri ya Congo(Brazzaville) Gabon, Ivory Coast, Liberia, Mali pamoja na Mauritania.

About the author

mzalendoeditor