Na Eva Godwin-DODOMA
Mtakwimu Mkuu Dkt.Albina Chuwa amewataka Watendaji, kata pamoja na Masheha baada ya mafunzo watakayopewa kwa muda wa siku mbili watakuwa na wajibu wa kushirikiana na kamati za Sensa na ngazi ya kata kufanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha kuwa zoezi la sensa linafanyika vizuri katika maeneo yao ya utawala
Ameyasema hayo leo Julai 28,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Takwimu Jijini Dodoma.
Amesema mambo ambayo wanatakiwa kuyafanya wakitoka katika mafunzo hayo ya siku mbili ni pamoja na kuongeza kasi ya uelimishaji na uamasishaji juu ya zoezi la Sensa.
“Mambo ambayo mnatakiwa kuyafanya baada ya mafunzo ya siku mbili ambapo siku ya tatu itakuwa tarehe 3 Agusti, ni kuendelea kuongeza kasi ya uelimishaji na uamasishaji katika suala la kushiriki Sensa kwa kutumia mbinu mbalimbali kama redio za kijamii ,ngoma, Mikutano na kuwashirikisha sekta binafsi katika sehemu husika”,amesema
“lakini pia jukumu la pili ni kuhainisha kaya za jumuiya kama vile hospitali, nyumba za kulala wageni, nyumba za mabweni kwa Wanafunzi na nyingine ambazo zinaweza kulaza watu zaidi ya elfu sita”.Amesema Chuwa
Hata hivyo amesema jukumu la tatu ni kuhainisha maeneo wanapolala Watoto au Watu wanaoishi mazingira magumu pamoja na Watu wanao hamahama kama vile wafugaji pamoja na kuainisha maeneo yote yenye mikusanyiko kama vile vituo vya daladala,stesheni za matreni, pamoja na sehemu vituo mbalimbali za usafiri.
Ameongezea kwa kusema Watu wanaoishi kwenye kambi za wakimbizi ni lazima wahesabiwe ikiwa wamelala ndani ya meeneo yao ya kiutawala
“Hakikisheni kuwa Watu wote wanaoishi kwenye kambi za wakimbizi wanahesabiwa ikiwa wamelala ndani ya maeneo yao ya kiutawala usiku wa muamkia siku ya Sensa
“Na jukumu la mwisho ni kushiriki kikamilifu katika kutoa usafiri kama vile pikipiki, boti, baiskeli na vifaa vingine vinavyofanana kwa lengo la kuwezesha zoezi la sensa kufanyika kwa wakati na kiufanisi”.Amesema
Ameongezea kwa kusema katika kipindi cha kuhesabu ambacho kitaanza tarehe 23 Agosti, 2022 watendaji wote wa kata na mashea kwa kushirikiana na wenyeviti wa vitongoji wa mitaa wote wanatakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makarani na wasimamizi wa sensa ikiwa ni pamoja na kuwatambulisha kwenye kaya na kuratibu shughuli zote za sensa
Amesema baada ya kuhesabu Watu tarehe 1-6 watendaji wote wa kata na kwa kushirikiana na wenyeviti wa vitongoji wa Wenyeviti wa Mitaa wote wanatakiwa kuhakiki idadi ya Watu wote katika maeneo yao ya kulala kwa kutumia mfumo wa kidigitali ambao utatolewa hivi karibuni.