Featured Kitaifa

RAIS DK.MWINYI AKABIDHI BOTI KWA WAVUVI NA WAKULIMA WA MWANI TUMBE NA KULIFUNGUA SOKO LA SAMAKI

Written by mzalendoeditor

BAADHI ya Vikundi vya Uvuvi Mkoa wa Kaskazini Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akiwahutubia kabla ya kukabidhi Boti kwa Wavuvi na Wakulima wa Mwani wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, zilizotolewa kwa Mkopo nafuu na Benki ya CRDB kwa Vikundi vya Ushirika, hafla hiyo iliyofanyika katika ufukwe wa Pwani ya Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi wa Tumbe wakati wa hafla ya kukabidhi Boti kwa Wavuvi wa Samaki na Wakulima wa Mwani wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba kutembelea Miradi ya Maendeleo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Hundi ya Milioni Mia Mbili na Kumi na Laki Nane Mwenyekiti wa Kikundi cha Uvuvi cha Kiuyu Mbuyuni Pemba.Ndg.Hatibu Khamis Faki ikiwa mkupo uliotolewa na Benki ya CRDB kwa kikundi hicho, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja Soko la Samaki Tumbe 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kulifungua Soko la Samaki Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba leo 26-7-2022, na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam, wakitembelea chumba cha kugandisha barafu katika Soko la Samaki Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba baada la kulifungua rasmin Soko hilo leo 26-7-2022, akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, kutembelea Miradi ya Maendeleo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Boti ya Uvuvi Kiongozi Ndg.Faki Mpemba Faki, kwa ajili ya Uvuvi wa Samaki, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Soko la Samaki Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba.(Picha na Ikulu)  

About the author

mzalendoeditor