Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Nnauye amezitaka menejimeti za wizara hiyo Kutathimini na kuangalia walipo toka, walipo sasa na wanapokwenda kwa kuweka mikakati mizuri ikiwa ni pamoja na kushikama,kupendana na kuwa na umoja utakasaidia wizara kupata mafanikio zaidi.
Nape alitoa rai hiyo kwa njia simu wakati akifungua mkutano wa mafunzo ya utendaji kazi kwa menejiment za mawasiliano na habari ambapo alisema kuwa angetamani kuona Upendo, mshikamano na umoja ikawa ndio msingi wa wizara hiyo hivyo watumie mkutano huo kufanya tathimini ambayo itawasaidia kuwa kundi na kuunganika pamoja kwani wao ni wizara ambayo inaangaliwa na kila mtu.
“Ni wajibu wetu sisi sote kuifanya wizara hii iwe ya umuhimu na ya maana, na naamini tathimini itayofanyika itatusaidia kuona jukumu la kila mmoja kuchangia kuifanya wizara iwe ya maana kwa kutoa mchango mkubwa kwa wizara zingine, nchi pamoja na watanzania kwani hatujawekwa hapa tulipo kwa bahati mbaya,” Alisema.
Alieleza ni vema kila mmoja akaona ana deni la kuacha alama kwenye nafasi walizopewa ili watu wakija kupitia kwenye sekta wawapongeze kwa mchango waliouacha, waweze kujivunia hata kama wamekaa kwa siku moja.
Kwa upande wake Naibu waziri wa habari mawasilia na teknolojia ya habari Mhandisi Kundo Methew alisema kuwa wameamua kufanya jambo ambalo ni la kipekee kwaajili ya menejimeti zao kwani ndio injinia ya wizara ambapo ni lazima waweke mipango ya kujitathimini ambapo pia wanaangalia Hali halisi ya utekelezaji wa bajeti yao ya 2021/2022 kujua wamefanya nini, ni wapi hawakwenda vizuri na wapi wamekwenda vizuri ili waweze kuyachukia mazuri hayo na kwenda nayo katika bajeti ya 2022/2023.
Mhandisi Kundo Alieleza katika mkutano huo taasisi zilizo chini ya wizara hiyo zote zimeweza kushiriki ambapo kila taasisi watawasilisha mafanikio na changamoto katika taasisi zao ili waingie mwaka unaokuja huku wakihakikisha wameyamaliza mapungufu yaliyokuwepo.
“Kikubwa ni tumefanya miradi mingi ndani ya wizara ikiwemo ujenzi wa mkongo wa taifa, utekelezaji wa anuani za makazi na posti code ambayo imefanyika kwa kiwango kikubwa ndani ya mwaka wa fedha 2021/2022 pamoja na mapinduzi ya kushirikiana na TANESCO katika kurekebisha kwa kushirikiana miundombinu ya mawasiliano kutoka kilometa 1880 ambayo hawakutumia bajeti waliyokiwa nayo ambapo kupitia fedha hiyohiyo wanaenda kujenga kilometa 4442,” Alieleza.
Alifafanua kuwa wamekuja kupanga mpango wa kutekeleza bajeti yao ambayo imeshapitishwa bungeni lakini pia kuangalia wapi walikosea na kurekebisha lengo ikiwa ni kuifanya Tanzania kuwa kituo cha TEHAMA na kuweza kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya mawasiliano kwa kuwa na wabunifu na wataalamu waliozalishwa hapa nchini.
Kwa upande wake mhariri mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN) Tuma Abdallah alisema kuwa mkutano huo itawasaidia kubadilishana mawazo lakini kuona ni namna bora ya kuboresha shughuli wanazozifanya pamoja na kushirikiana katika kupeleka mbele maendeleo ya taasisi zao.