Featured Kitaifa

MWENGE WA UHURU WATUA KWENYE KIWANDA CHA BIA CHA GAKI SHINYANGA

Written by mzalendoeditor

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma akitembelea Kiwanda cha Bia Gaki Investment Co. Ltd.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma amewasili katika Kiwanda cha Bia Gaki Investment Co. LTD na kuweka Jiwe la Msingi, na kupongeza kwa uwekezaji mkubwa ambao utatatua changamoto ya Ajira kwa Vijana na kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa na Taifa kwa ujumla.

Mwenge huo wa Uhuru umewasili leo Julai 27, 2022 Kiwandani hapo na kukagua Kiwanda hicho na kuridhishwa na uwekezaji huo na kisha kuwekwa Jiwe la Msingi.

Geraruma amesema Mradi huo wa Kiwanda cha Uzalishaji Bia ni mzuri, na kupongeza uwekezaji huo mkubwa, ambao unaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya viwanda.

“Uwekezaji huu ni mkubwa siyo wa kitoto, nakupongeza sana Gaspar Kileo ‘Gaki’ kwa kuunga mkono Sera ya Viwanda, na Kiwanda hiki kitasaidia kutatua changamoto ya Ajira na kukuza uchumi,” amesema Geraruma.

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Sekta Binafsi ili kuhakikisha uchumi wa Mtu Binafsi unakua na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, amepongeza uwekezaji huo ambao utatoa ajira nyingi kwa vijana.

Meneja wa Kiwanda hicho cha Bia Gaki Investment Co. Ltd Reonald Mushi, amesema ujenzi wake ulianza mwaka 2019 na unatarajiwa kukamilika mwaka huu kwa gharama ya Sh.bilioni 33.4 na utatoa ajira rasmi kwa vijana 150.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Sahili Nyanzabara Geraruma akizungumza kwenye Kiwanda cha Bia cha Gaki Investment Co Ltd.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, akizungumza katika Kiwanda cha Bia Gaki Investment Co Ltd.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye Kiwanda hicho cha Bia Gaki Investment Co Ltd.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akiwa katika Kiwanda cha Bia Gaki Investment Co Ltd

Muonekano wa Mitambo ya Uzalishaji wa Bia katika Kiwanda cha Gak Investment  Co Ltd

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Bia Gaki Investment  Co Ltd, Gaspar Kileo (Gaki) akionesha mitambo ndani ya kiwanda hicho.





Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akiwa katika Kiwanda cha Bia Gaki Investment  Co Ltd

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akiweka Jiwe la Msingi katika Kiwanda cha Bia Gaki Investment  Co Ltd

Jiwe la Msingi.
Muonekano wa baadhi ya majengo katika Kiwanda cha Bia Gaki Investment  Co Ltd

Bango la Mwenge wa Uhuru katika Kiwanda cha Bia Gaki Investment  Co Ltd

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa akiwa Katika Kiwanda cha Bia Gaki Investment Co Ltd.

About the author

mzalendoeditor