Featured Kitaifa

LATRA YAPIGA MARUFUKU MAHUBIRI,BIASHARA,MZIKI MKUBWA KWENYE MABASI

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA ) Habibu Suluo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 26,2022 jijini Dodoma  kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa Barabara Johansen Kahatano,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 26,2022 jijini Dodoma wakati LATRA wakitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Mkurugenzi wa udhibiti Usafiri wa Reli Mhandisi Hanya Mbawala,akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 26,2022 jijini Dodoma wakati LATRA wakitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

………………………………

Na Eva Godwin-DODOMA

SERIKALI kupitia  Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA ) imepiga marufuku mahubiri , biashara ,mziki Mkubwa na picha zisizo na Maadili kufanyika ndani ya vyombo vya usafiri ambavyo vinasababisha usumbufu kwa abiria.
Hayo yamesemwa leo Julai 26,2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA ) Habibu Suluo,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Amesema kuwa baadhi ya vyombo vya usafiri zimekuwa zikikeuka miiko ya usafirishaji na kutoa rai kwa abiria kutoa taarifa mapema endapo gari walilopanda linaruhusu huduma hizo kuendelea ndani ya basi huku safari ikiwa inaendelea.
Bw.Suluo amesema ni marufuku huduma hizo ndani ya mabasi kufanyika kwani zimekuwa zikileta hisia tofauti kwa sababu kila msafiri anaimani tofauti tofauti.
“Tuzingatie Kanuni taratibu na miongozo izlizowekwa na  LATRA, mahubiri ndani ya mabasi hayaitajiki na endapo ikabainika basi linafanya huduma hiyo hatua Kali za kisheria zitachukuliwa kwa dereva na Mmiliki wa gari hilo,” Bw.Suluo 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa Barabara Johansen  Kahatano ,amesema kuwa ni kosa kisheria kwa mabasi kuwabagua abairi  na endapo ikitokea mtu akafanya  kitendo hicho apekeke malalamiko yake katika mamlaka husika.
” Tuliseme hili wazi Serikali ndio iliyokuwa na mamlaka ya Kutoa huduma ya usafirishaji lakini Serikali ikawapa jukumu hilo sekta binafsi,badala  ya Serikali kutoa huduma wenyewe imewaachia sekta binafsi Kutoa huduma ya usafiri hivyo vitendo vya kubagua abiria vuachwe mara moja kwani abiria wote ni wananchi,” amesema Kahatano

About the author

mzalendoeditor