Featured Michezo

KMC YATOA UFAFANUZI KUHUSU KUACHWA KWA WACHEZAJI

Written by mzalendoeditor

Wachezaji wa Timu ya KMC FC tayari wameshawasili kambini kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea katika msimu mpya wa 2022/2023 utakaoanza Agost 17 mwaka huu kwa mujibu wa ratiba ya Bodi ya ligi Kuu Tanzania TPLB.

Wachezaji waliowasili kambini hadi sasa ni maingizo mapya waliosajiliwa msimu huu, nawaleambao walikuwa kwenye mipango ya kocha Mkuu Thierry Hitimana mara baada ya kumalizika kwa msimu wa 2021/2022.

KMC kwasasa itaweka kambi yake hapa Jijini Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya huku ikiendelea kujifua zaidi kutokana na programu ambazo kocha mkuu Hitimana ameandaa  kwa ajili ya kuwajenga wachezaji kabla ya kuanza kwa msimu mpya Agost 17.

Katika kipindi hiki cha maandalizi ya msimu Mpya (Pre- seanson ) kwa mujibu wa program ya kocha Hitimana kutakuwa na mechi nyingi za kirafiki, mazozi ya uwanjani kwa awamu mbili ambazo ni uwanjani pamoja na Gym.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni  hadi sasa imeachana na wachezaji 10 ambao ni Hassan Kesssy, Hassan Kabunda, Ally Ramadhani Oviedo, Sudi Dondola, Denis Richard, Jeani Mugiraneza,Hassan Kapalata, Nickson Kibabage, Martin Kigi pamoja na Abasi Kapombe.

KMC FC ilifikia uamuzi wa kuachana na wachezaji hao ambapo baadhi walikuwa wamemaliza mikataba yao huku wengine uongozi ukiwapa nafasi ya kutafuta changamoto nyingine na kwamba tayari imeshakamilisha usajili wa wachezaji wengine ambao wataanza kutambulishwa muda wowote kuanzia sasa.

About the author

mzalendoeditor