Featured Kitaifa

DUWASA YABAINISHA MIKAKATI YAKE YA KUMALIZA KERO YA MAJI JIJI LA DODOMA

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA),akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 25,2022 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari maelezo Gerson Msigwa,akizungumza wakati Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA),ikiwasilisha utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 leo Julai 25,2022 jijini Dodoma.

Mwandishi kutoka Gazeti la Mwananchi Sharon Sauwa,akiuliza swali  wakati wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA),wakiwasilisha utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 leo Julai 25,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA),akijibu maswali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 25,2022 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

.………………………..

Na Eva Godwin-DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) ipo katika hatua za mwisho za kumpata Mkandarasi Mshauri kwa ajili ya mradi wa uboreshaji wa huduma Maji taka jijini Dodoma.

Hayo ameyasema leo Julai 25,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na  waandishi wa habari  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/23

Amesema kuwa Mradi huo utaweza kutibu Maji taka lita milioni 20 kwa siku,ujenzi wa mabwa 16 eneo la Nzuguni,Utaongeza mtandao wa Maji taka usiopungua kilomita 250,utaunganisha wateja wasiopungua 6,000 na
Utaongeza huduma ya usafi wa Mazingira kutoka asilimia 20 hadi 45.

” Mradi wa Maji taka na uboreshaji huduma ya Maji safi kwenye Mji wa Serikali ambao unashughulikiwa na Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kushirikiana na DUWASA ipo katika hatua za mwisho kusaini mkataba na unagharimu takribani shilingi Bilioni 94, ambazo zimeshatengwa na Serikali Kuu”,amesema

“Dodoma kwa sasa imekuwa sana tofauti na miaka ya nyuma na ndio maana sisi kama DUWASA tunafanya kila jitihada za kuboresha miundombinu ya maji safi na majitaka kwa sababu ukiangalia hata idadi ya majengo na watu imeongezeka na kila nyumba inahitaji majisafi na miundombinu bora ya majitaka na ndio maana tunapambana kutaka kutekeleza Miradi hiyo”.Amesema Aron

Ameongezea kwa kusema Upatikanaji wa maji safi Mkurugenzi huyo amesema kuwa kwa makadirio yaliyopo Mamlaka hiyo inahudumia zaidi ya wakazi – 500,000 ambapo wanaopata Majisafi ni asilimia themanini na mbili (82%).

“Niwaambie tu ndugu waandishi kwa sasa tuna wakazi laki tano 500000 tunaowahudumia na Mahitaji ya maji
lita milioni 133 kwa siku (Mwaka 2022) na yataongezeka hadi lita milioni 204 kwa siku (mwaka 2036)”amesema

“Kwa hiyo Wateja wetu jitahidini kulipa Ankara (bill) zenu za Maji usisubiri mpaka deni liwe kubwa alafu ndio uje kulipa baada ya kukatiwa maji hivyo unaatutafutia lawama tu alafu kingine mmekuwa wazito sana kuja kuhakiki bili zenu pindi mnapopata ujumbe mfupi ambao umekuwa unatumwa katika simu zenu ninawaomba mjitahidi kujenga tabia ya kuhakiki kabla hujalipa ili kujiridhisha ni kweli bili uliyopewa ni sawa na matumizi yako? ” .Amesema Aron

Naye Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari maelezo Gerson Msigwa ametoa pongezi kwa mamlaka hiyo akisema kuwa wamejitahidi kuboresha upatikanaji wa maji safi ukizingatia na kasi ya ukuaji wa mkoa wa Dodoma.

“Niwapongeze tu DUWASA kwani mmeonesha mfano mzuri kivitendo kwani pamoja na serikali kuhamia Dodoma kikamilifu bado mmesimama imara na mpaka sasa mnaendelea kuhakikisha huduma ya maji katika jiji la Dodoma inaboreshwa kulingana na idadi kubwa ya watu iliyoongezeka kwa kipindi kifupi” amesema Msigwa

“Kumtua Mama ndoo kichwani ni jukumu ambalo Mhe.Rais Samia amelibeba hivyo kupitia mamlaka mbalimbali za Maji safi na usafi wa mazingira kutoka Mikoa yote imsaidie Mhe.Rais kutimiza adhma hiyo.

About the author

mzalendoeditor