Featured Kitaifa

OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA YAPOKEA HATI YA USHINDI WA USAFI WA OFISI ZA WAKUU WA MIKOA NCHINI

Written by mzalendoeditor

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga, amekabidhiwa hati ya ushindi wa Usafi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa nchini. Dkt Mganga amekabidhiwa hati hiyo ambayo ilipatikana katika mashindano yaliyofanyika Mwaka 2021.

Hati hiyo ya usafi imetolewa na Wizara ya Afya imewasilishwa leo kwa Katibu Tawala
Mkoa wa Dodoma na Ndugu Joseph Birago ( kwenye picha mwenye suti nyeusi).

Ofisi ya Mkoa wa Dodoma imepokea hati hiyo mara baada ya kushika nafasi ya tatu kati ya ofisi za Mikoa 26 nchini katika mashindano yaliyofanyika mwaka 2021.

Akipokea hati hiyo
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga, amesema usafi wa mazingira katika ngazi ya Kaya na Taasisi kwa sasa ni kipaumbele cha Mkoa. Dkt. Mganga amemshukuru sana Mheshimiwa Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kukusanyia taka ngumu katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kwingineko.

About the author

mzalendoeditor