Featured Kitaifa

RC MTAKA ATOA SIKU 7 WANANCHI WALIOJIANDIKISHA KUDAI FIDIA ZA ARDHI KWA UDANGANYIFU KUONDOA MAJINA YAO HARAKA

Written by mzalendoeditor

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza na viongozi wa mkoa pamoja na watumishi idara ya ardhi  kuhusu tamko kuhusiana na madai ya viwanja  vya Msalato leo Julai 22,2022 jijini Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,akizungumza wakati wa kikao na viongozi wa mkoa pamoja na watumishi idara ya ardhi  kuhusu tamko kuhusiana na madai ya viwanja  vya Msalato leo Julai 22,2022 jijini Dodoma.

Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatma Mganga,akizungumza wakati wa kikao na viongozi wa mkoa pamoja na watumishi idara ya ardhi  kuhusu tamko kuhusiana na madai ya viwanja  vya Msalato leo Julai 22,2022 jijini Dodoma.

Kamishna wa Ardhi Jiji la Dodoma ,Thadei  Kabonge ,akizungumza wakati wa kikao na viongozi wa mkoa pamoja na watumishi idara ya ardhi  kuhusu tamko kuhusiana na madai ya viwanja  vya Msalato leo Julai 22,2022 jijini Dodoma.

Sehemu ya viongozi wa mkoa pamoja na watumishi idara ya ardhi  wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka.

…………………………………..

Na Eva Godwin.DODOMA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka, amewataka Wananchi Mkoani Dodoma walio Vamia maeneo ambayo serikali imetwaa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kitaifa na kujirodhesha kudai fidia katika uwanja wa Ndege wa Msalato kwa njia ya udanganyifu, kufika katika ofisi za mtaa kuondoa majina yao haraka .

Hayo ameyasema hayo leo Julai 22,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na viongozi wa mkoa pamoja na watumishi idara ya ardhi  kuhusu tamko kuhusiana na madai ya viwanja  vya Msalato.

Amesema kwa mujibu wa sheria ya kanuni za Adhabu sura ya 16 toleo la 2019,kifungu 301 na 302 ni kosa la jinai kufanya udanganyifu kwa lengo la kujipatia fedha za serikali, adhabu ya hatia hii ni jela miaka 7, sambamba na jela kwa mujibu wa kifungu cha 31 sura ya 16 toleo la 2019, Mahakama yaweza kukuamuru ulipe fidia kwa madhara uliosababisha kwa Serikalu kupitia udanganyifu wako.

“Ninatoa siku saba kuanzia leo tarehe 22 Julai, 2 hadi 29 Julai, 2022 Kuondoa majina ndani ya siku hizo bila kuchukuliwa hatua yoyote ya kisheria”,amesema

“Watakao kaidi wito huu timu yangu itafanya msako mkali kubaini wanaodanganya kwa nia ya kujipatia fidia isiyo halali na kuingiza serikali hasara watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufungwa jela miaka saba”.Amesema mtaka

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amesisitiza wanunuzi wa ardhi wa Jiji la Dodoma watambue mamlaka ya upangaji ni mkurugenzi wa Dodoma, kwa mujibu wa kuzingatia sheria na kanuni za ununuzi.

“Ni muhimu kujiridhisha eneo ambalo unalinunua tena ukiwa na mkurugenzi wa Dodoma kinyume cha hapo utajiingiza kwenye migogoro na susi serimali unatutia kwenye changamoto hiyo”,amesema

“Tumekuwa tukichukua hatua kwa watumishi wa umma na wako watumishi wamesimamishwa kazi na bado wapo mitaani na pia wale wanaowasababishia watumishi wetu kuingia kwenye ulaghai tumeshawachukulia hatua”.Amesema Shekimweri

Naye  Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatma Mganga,amesema Serikali inakumbukumbu kwa kila mtu aliyelipwa fidia hivyo kuwa makini katika suala la kutaka kulipwa fidia kwa kugeuza majina

“Serikali ilianza kulipa fidia kutoa eneo kujenga uwanja wa kimataifa tangu 2008 na Baadhi ya Wananchi walilalamika hawakulipwa fidia na hapo Serikali ilisikia na 2012 na 2019 Ilitoa tena fedha nyingi kulipa fidia, lakini sahivi kuna wimbi kubwa la watu limejitokeza kutaka kulipwa fidia”,amesema

“tunaomba sana kama umetumia njia aramu ya kuomba fidia naomba futa jina mapema tumtii Kiongozi wetu wa mkoa ili tuendelee na shughuli nyingine za kimaendeleo Mkoani kwetu”.Amesema Mganga

Naye Kamishna wa Ardhi Jiji la Dodoma ,Thadei  Kabonge amesema sheria itachukua mkondo wake kwa wale wasio waaminifu katika kukiuka sheria na taratibu zilizopangwa.

About the author

mzalendoeditor