Featured Kitaifa

RC MTAKA ATOA MAAGIZO KWA WAKUFUNZI WA MAKARANI WA SENSA

Written by mzalendoeditor

MKUU wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza kwenye  kikao Cha wakufunzi wa Sensa kutoka  wilaya zote za mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo Julai 22,2022 jijini Dodoma.

……………………

Na Eva Godwin-DODOMA

MKUU wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amewaagiza wakufunzi wote waliochaguliwa  kutoa mafunzo kwa makarani wa sensa kuhakikisha wanazingatia  uadilifu pamoja na weledi wa taifa ili kuweza kumsaidia Mhe . Rais Samia katika kuyafikia yale ambayo yanakusudiwa kupatikana katika zoezi la sensa.

Agizo hilo amelitoa leo Julai 22,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye  kikao Cha wakufunzi wa Sensa kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Dodoma,Mtaka  amesema kuwa ni vizuri kujuwa kwamba wamebeba dhamana kubwa na majukumu ya serikali ili kuhakikisha zoezi hilo la sensa linakwenda salama.

Amesema kuwa suala la sensa linalindwa na Sheria ili ikitokea karani akaharibu zoezi hilo atahukumiwa kifungo Cha miezi sita na kuendelea, kwakuwa sensa ni jukumu ambalo linalindwa na sheria za nchi.

“Matarajio yangu mtafanya kazi vizuri na tutaona fahari katika mkoa wa Dodoma na wale ambao ni watumishi mfanye kazi msije kufanya ya Ngoswe”,amesema

“Nyie ni watu mema mtafanya kazi vizuri na tunaweka kumbukumbu mkitupa ufahari na mtatusaidia malengo yetu yaende vizuri katika suala la sensa katika Mkoa wetu wa Dodoma”.Amesema Mtaka

Naye,Katibu tawala Mkoa wa Dodoma Dk. Fatma Mganga , amesema kuwa watakao sababisaha mkoa wa Dodoma kufanya vizuri katika Sensa ni wakufunzi ambao wataenda kuwafundisha makarani, ambao kila mkufunzi atakuwa anafundisha makalani 70.

” Zoezi la sensa ni nyeti katika ustawi wa taifa la Tanzania hivyo tunapaswa kuwa waadilifu na kuzingatia maadili pamoja na kusimamia vizuri zoezi hili la Sensa

“Mmeteuliwa kufanya jukumu muhimu na nyeti sana nyinyi mtatufanya tufanye vizuri katika zoezi la Sensa, Sensa ni Afya sensa ni elimu sensa ni Maji na Sensa ni barabara, na hili ni swali la Wananchi wengi na nyinyi ndio mtaenda kujibu maswali haya, hili zoezi haliitaji masihara zoezi hili ni la kiusalama kwa taifa Letu”.Amesema Mganga

Mfunzo hayo yalianza tangu tarehe 6 mwezi huu ambapo ni takribani siku 17, ambayo yanawahususha washiriki 415 kutoka katika halmashauri zote za Jiji la Dodoma.

About the author

mzalendoeditor