Featured Kitaifa

VYUO VIKUU NA KATI VYAAGIZWA KUKAMILISHA UANZISHWAJI WA MADAWATI YA JINSIA KUFIKIA DESEMBA

Written by mzalendoeditor

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akizindua Dawati la Jinsia katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akipokea daftari la kurekodi kumbukumbu za matukio ya ukatili wa kijinsia kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la UNESCO Mathias Herman wakati wa uzinduzi wa Dawati la Jinsia Chuo Kikuu cha Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akikabidhi Daftari la kurekodi kumbukumbu ya matukio ya ukatili wa kijinsia kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Professa Faustine mara baada ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa James Mdoe akitoa salamu za Wizara hiyo katika hafla ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) 

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Professa Faustine Bee akizungumza wakati wa uzinduzi wa Dawati la Jinsia Chuoni ha

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akizungumza wakati wa uzinduzi wa Dawati la Jinsia katika Chuo Kikuu cha Dodoma

Baadhi ya wanafunzi na watumishi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakishuhudia uzinduzi wa Dawati la Jinsia Chuoni hapo

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju (katikati waliketi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Dawati la Jinsia la Chuo Kikuu cha Dodoma mara baada ya kuzindua dawati hilo Julai 22, 2022.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM

…………………………..

Na WMJJWM, Dodoma

Vyuo Vikuu na vya Kati nchini ambavyo havina madawati ya Jinsia vimetakiwa kuhakikisha kufikia Mwezi Desemba viwe vimeanzisha madawati hayo.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju wakati akizindua Dawati la Jinsia katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Julai 22, 2022.

Mpanju ambaye ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Professa James Mdoe, amemuomba Wizara hizo zishirikiane kuhakikisha madawati 612 yanaanzishwa katiia Vyuo kufikia Desemba mwaka huu.

“Tusisubiri wabia watufadhili ndiyo tuzindue, kufikia Desemba Vyuo Vikuu na Vyuo vya kati vyote kuwa na madawati kwa rasilimali zilizopo kwa sababu mwongozo upo na

lengo ni kutoa wahitimu waliofuzu bila kuathiriwa na vitendo vya ukatili au unyanyasaji wa kijinsia” alisema Mpanju.

Mpanju amekipongeza Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kuwa na utaratibu wa kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kabla hata ya mwongozo wa Wizara wa uanzishwaji wa madawati hususani Kaulimbiu inayowataka kutovumilia unyanyasaji huo na kuvitaka Vyuo vingine kuiga mfano huo.

“Kuwa na sera na miongozo ya kupinga vitendo vya ukatili kabla ya uzinduzi wa Dawati zinadhihirisha utayari wa Chuo hiki kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia” alisema Mpanju

Amelishukuru pia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kusaidia uzinduzi wa madawati 15, vilevile kuona ukubwa wa Chuo cha Dodoma na kuamua kuzindua madawati mawili katika Chuo hicho.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe alisema Wizara ya Elimu ilishatoa maelekezo ya kuwa na sera na miongozo vyuoni pamoja na kuanzisha madawati ya Jinsia hivyo watahakikisha wanasimmaia Vyuo hivyo ili vianzishe madawati hayo na yatumike kama Mwongozo wake unavyokusudia.

“Sote tunakubaliana kuwa, yakiwepo manyanyaso ya kijinsia wanafunzi hawawezi kutimiza lengo lao. Hivyo nielekeze Vyuo vingine kuanzisha madawati haya kwa namna yoyote iwe kwa kushirikiana na Wadau au kwa kutumia rasilimali za ndani” alisisitiza Prof. Mdoe.

Naye Mwakilishi wa UNESCO Mathias Herman alisema Shirika lilo linatambua juhudi zinazofanywa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wnawake na Makundi Maalu na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  hasa katika kutoa miongozo ya uanzishwaji wa madawati ya Jinsia na kuisimamia kuhakikisha inafanya kazi.

Aidha Bw. Mathias alisema madawati haya sio tu kwamba yanazinduliwa bali yanakuwa na tija kwa kuwasaidia jumuiya yote ya wanachuo kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na hatimaye kutokomeza vitendo hivyo katika Taasisi hizo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Faustine Bee alisema uanzishwaji wa Dawati hilo chuoni hapo utasaidia kuongeza ufanisi wa Kitengo cha Jinsia kilichoanzishwa mwaka 2009 Chuoni hapo.

Aliongeza kwamba, Chuo kinatambua usawa kijinsia na ndiyo sababu tangu kitengo hicho kianzishwe kimekuwa kikifanya kazi ya kupinga na kupambana na vitendo ya ukatili ndani na nje ya Chuo kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo makongamano, mafunzo na Utafiti wa namna ya kupambana na vitendo hivyo.

“Tutahahakikisha tunatekeleza kwa ufanisi uendeshaji wa shughuli zilizopangwa chini ya Dawati hili na kutoa taarifa ya yote yanayojiri Dawatini hii itaimarisha zaidi kitengo cha Jinsia na kufanya Chuo kuwa mahali salama kwa kuzingatia usawa wa kijinsia” alisema Prof. Bee.

Hafla ya uzinduzi wa Dawati hilo imeenda sambamba na Naibu Katibu Mkuu Amon Mpanju kukabidhi Madaftari 800 kwa ajili kurekodi kumbukumbu za matukio ya ukatili vyuoni.

About the author

mzalendoeditor