Featured Kitaifa

RC MAKALLA ATOA WITO KWA WADAU KUCHANGIA VIFAA VYA USAFI

Written by mzalendoeditor
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Amos Makalla leo amepokea Vifaa vya Usafi kutoka Kampuni ya usafirishaji ya 
TOSH ambayo imejitolea kuunga mkono Serikali katika Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM.
Akipokea Vifaa hiyo RC Makalla ameishukuru TOSH CARGO kwa kuguswa kutoa msaada huo na kutoa wito kwa Wananchi na Wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi kutoa msaada wa Vifaa vya ili kulifanya Jiji kuwa safi na la kuvutia.
Aidha RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi Julai 30 kwenye Usafi wa Barabara kuu za Mkoa huo huku akibainisha Mpango wa kutenga baadhi ya maeneo kwaajili ya Ujenzi wa (Fountains) ikiwemo sehemu za (round about).
Pamoja na hayo RC Makalla amesema kwa mwenendo na mwamko mzuri ulioonyeshwa na Wananchi ni wazi kuwa Dar es salaam itakwenda kutoka nafasi ya sita kwa Usafi Barani Africa na kushika nafasi za juu zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TOSH CARGO Mohamed Nassor amesema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika jitiada za RC Makalla za kuifanya Dar es salaam kuwa safi.

About the author

mzalendoeditor