Featured Michezo

MANARA AFUNGIWA MIAKA MIWILI NA FAINI MILIONI 20

Written by mzalendoeditor

KAMATIĀ  ya Maadili ya TFF imemhukumu Ndugu Haji Manara kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kipindi cha miaka miwili (2) na kutozwa faini ya Tsh. Milioni 20 [Tsh 20,000,000] kwa makosa ya kumvunjia heshima Rais wa TFF Wallace Karia Adhabu hiyo inaanza leo Alhamisi, Julai 21, 2022.

Haji Manara alipishana kauli ya Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia katika eneo la VVIP wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la ASFC kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union.

About the author

mzalendoeditor