Featured Kitaifa

IGP WAMBURA:’WATAKAOVUNJA SHERIA KUSHUGHULIKIWA’

Written by mzalendoeditor

Na Mwandishi Wetu-ARUSHA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camilus Wambura amewataka wananchi wa jiji la Arusha kuendelea kutunza amani iliyopo na kutokujiingiza kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani hasa kipindi hiki ambapo kuna mkutano mkubwa wa Maras kutoka nchi saba za afrika mashariki.

IGP Wambura amesema hayo baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Polisi mkoa wa Arusha na kupokelewa na kamanda wa Polisi mkoani humo Justin Masejo ambapo aliwataka askari kuendelea kusimamia amani na kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kutaka kuvuruga amani ya nchi.

Na kuahidi kushughulika na yeyote ambaye atakuwa na vitendo vyovyote kinyume na maadili na kinyume na matendo mema ya Watanzania.

About the author

mzalendoeditor