Featured Kitaifa

MIFUGO 1448 YAKAMATWA KWA UHARIBIFU WA MAZAO

Written by mzalendoeditor

Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi

Kamanda wa kikosi cha kuzuia  wizi wa mifugo na migogoro ya mifugo  Tanzania kamishina msaidizi wa Polisi  ACP – simon Pasua kizungumza na vyombo vya habari leo 18 Julai 2022 amesema kuwa mnamo tarehe 09 Julai  2022 huko maeneo ya kijiji cha Olmolog katika halmashauri ya wilaya siha Mkoa wa Kilimanjaro walifanikiwa kukamata mifungo ipatayo 1448 ambayo  ili haribu  jumla ya ekari 387 ya mashamba ya wakulima yenye mazao tofauti tofauti yenye thamani  ya Tsh. 166,290,000/= milioni mia moja sitini na sita na laki mbili na tisini.

Kamanda Pasua ameitaja mifugo hiyo kuwa  ni ng’ombe 485,mbuzi na kondoo jumla yake ni 963 ambapo ameleza kuwa mifugo hiyo ili haribu ekari hizo za mazao na  uchunguzi wa awali umebaini kuwa mifugo hiyo imetoka nje ya mkoa wa Kilimanjaro na kuingia katika wilaya ya siha bila ya kufuata utaratibu .

Aidha amesema mifugo iyo ilikamatwa na hakuonekana mmiliki wa mifugo hiyo mpaka taratibu za kimahakama zilipo kamilika na umuazi kutolewa juu ya uharibifu wa mazao hayo ambapo mahakama ya wilaya siha ilitoa hukumu kuwa mifugo hiyo itaifishwe.

Kamanda Pasua ametoa wito kwa wafugaji kutoka leta migogoro baina yao na wakulina na badala yake amewaomba kufuata maeneo yaliyotengwa kwa ajili kwa kulisha mifugo yao na kuepusha migogoro baina yao na wafungaji

About the author

mzalendoeditor