CHAMA Cha Mapinduzi @ccmtanzania Kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa zamani wa Chama Cha Wananchi (CUF) na Mkurugenzi wa Fedha na Mipango Bi Khadija Makontena kilichotokea Alhamisi 14 Julai, 2022.
Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan amemtumia salaam za pole Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF ) Profesa Ibrahim Lipumba, familia, ndugu na jamaa.
“Bi Khadija tokea kuanzishwa mfumo wa Vyama Vingi vya siasa amekuwa akishiriki kikamilifu katika uwanja wa siasa za ndani na nje ya chama chake huku akiamini siasa za umoja na maelewano.” Ndugu Samia Suluhu Hassan
Mwenyezi Mungu awape ustahamilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Sisi Sote niwa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
Shaka Hamdu Shaka
Katibu Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
14 Julai, 2022