Featured Kitaifa

MBUNGE SALIM ALMAS AMALIZA CHANGAMOTO YA MAJI NAKAFURU – KATA YA LUPIRO ACHIMBA VISIMA 5 WANANCHI KICHEKO

Written by mzalendoeditor

MBUNGE
wa Jimbo la Ulanga (CCM) Mhe Salim Alaudi Hasham ametatua  ya
changamoto ya miaka mingi ya kukosa maji safi na salama kwa wananchi
wa kijiji cha Nakafuru kata ya Lupiro wilayani Ulanga ambapo kwa sasa
wakazi wake wananufaika na huduma hiyo
Wananchi
hao walimuomba mbunge wa Jimbo hilo awatatulie changamoto hiyo kwani ni
adha kubwa jambo linalopelekea kina mama na watoto kuteseka kufuata
maji kwa umbali mrefu na wakati mwengine kunywa maji yasiyo salama jambo
linalohatarisha maisha yao kwani Afya zao zinakuwa matatani.
Mbunge huyo baada ya kusikia kilio hicho
akatoa kiasi cha Shilingi milioni 2.5 kwaajili ya uchimbaji wa visima
vitano na utengenezaji wa miundombinu ya bomba ili maji yapatikane kwa
uhakika bila changamoto.
Zoezi
la uchimbaji wa visima limekamilika na mapema katibu wa mbunge wa jimbo
hilo Ndugu Thomas Justice Daffa amewakabidhi wananchi visima hivyo na
kuwataka wavitumie kwa umakini kwa kuvitunza ili viwasaidie kwa muda
mrefu.
Visima hivyo
vilivyochimbwa na kampuni ya Msabi pia vitakuwa nanutaratibu wa
kufanyiwa matengenezo mara kwa mara na kampuni hiyo ili kuhakikisha
wananchi wa eneo hilo hawakosi maji safi na salama wakati wote.
Baada
ya kukabidhiwa visima hivyo wananchi wa eneo hilo walimshukuru mbunge
kwa msaada huo mkubwa kwani kilio hicho kilikuwa cha miaka mingi na
walimuomba aendelee na moyo hio wakuwasikiliza wananchi wake na
kuwatatulia changamoto zao zinazowakabili.
Penye
mafanikio hapakosi changamoto wanachi hao baada ya kupata maji
wakaendelea kumuomba mbunge awapambanie kupata umeme wa uhakika katika
baadhi ya vitongoji vyao ambavyo havijafikiwa na umeme jambo ambalo
linawarudisha nyuma kimaendeleo kwani wanashindwa hata kufanya biashara
ndogo ndogo kwa kukosa huduma hiyo.
Katibu
wa Mbunge Ndugu Thomasi Justice Daffa kwaniaba ya mbunge aliwaahidi
kulibeba swala hilo na kulisimamia kidete ili nishati hiyo muhimu
iwafikie wananchi wote wa nakafuru.

About the author

mzalendoeditor