Featured Kitaifa

WATU WATATU WAFARIKI LINDI KWA UGONJWA USIO WA KAWAIDA

Written by mzalendoeditor

Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichwale ,akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma  kuhusu Ugonjwa usio wa kawaida.

………………………………..

Na Eva Godwin-Dodoma

SERIKALI kupitia wizara ya afya imesema Mkoani Lindi halmashauri ya Ruangwa katika kituo cha afya cha Mbenyekera tarehe 12 Julai wamepokea taarifa ya wagonjwa watatu kufariki na ugonjwa usio wa kawaida wa kuvuja damu hususani puani,kichwa kuuma na mwili kuchoka sana ulijitokeza june 7 mwaka huu ikiwa wagongwa wengine10 wakiendelea na matibabu .

Hayo yameelezwa leo Julai  13, 2022 na Mganga Mkuu Wa Serikali Dkt.Aifello Sichale wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma.

Amesema timu ya wataalamu inaendelea na uchunguzi wa ugonjwa huo ili kubaini aina ya ugonjwa huo ambao umekuwa

” Tarehe 7 Juli mwaka huu Tulipata taarifa kwa mganga mkuu mkoa wa lindi katika Almashauri ya luwangwa kumejitokeza na ugonjwa usio wa kawaida katika kituo cha Afya cha Mbenyekela ambapo walipokea wagonjwa wawili ambao walikuwa wakisumbuliwa na kichwa kuuma,damu kutoka puani na mwili kuchoka, na Julai 12 tumepokea taarifa ya vifo vya watu watatu waliofariki na ugonjwa huo usio julikana”, amesema

“Wizara ya Afya tumeunda timu ya wataalamu kutoka kwenye idara ya magonjwa ya dharura na pia katika taasisi mbalimbali za utafiti pamoja na timu ya almashauri ya Luwangwa na timu zipo zinaendelea na kazi”.Amesema Sichale

Aidha Dkt. Sichalwe ametoa wito kwa wananchi kwa watulivu wakati serikali ikiendelea kulifanyia kazi suala hili pamoja na wanachi kuendelea kutumia vituo vya kutolea huduma za afya pale wanapojisikia kuumwa.

“Wananchi tuwe watulivu huku wizara ikiendelea kufanyia uchunguzi suala hili na pia tunatoa wito kwa Wananchi wote ukijiisi unadalili hizo fika katika vituo vya huduma ya afya mapema

“Pia unaweza ukawamshauri kwa Mtu ambae unaona anadalili kama hizo afike katika kituo cha afaya mapema ili apate huduma”.Amesema Sichalwe

About the author

mzalendoeditor