Featured Kitaifa

AJALI:WATU NANE,WATANO FAMILIA MOJA WAFARIKI KWA AJALI YA GARI

Written by mzalendoeditor
Na Silvia Mchuruza,Biharamulo,Kagera.
WATU nane wamefariki Dunia kwa ajali ya Gari lenye namba za usajili RAF 129W ikiwa ni treila lenye namba za usajili RL 4367 Aina ya Mercedes Benz watano wakiwa ni familia moja Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera 
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa Jeshi la polisi  ACP William .T. Mwampagale amesema  ajali iliyotokea July 11 mwaka huu katika maeneo ya Busiri  katika barabara kuu ya  kutoka Lusahunga kuelekea Nyakahuru wilaya ya Biharamulo imesababisha vifo vya watu nane na watano wakiwa Ni familia moja.
Aidha amesema kuwa ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili RAF 129W ikiwa ni treila lenye namba za usajili RL 4367 Aina ya Mercedes Benz lililokuwa likiendeshwa na  Vicent Gakuba (52)mnyarwanda  mkazi wa nyamata rugesela East province Rwanda kigari ambapo gari hiyo ilikuwa ikitokea rwanda kuelekea jijini Dar es salaam.
Pia ameongeza kuwa gari Hilo liligongana uso kwa uso na  gali lenye namba T.626 DRX  Aina ya Toyota succeed lililokuwa likiendeshwa na ndg. Nyawenda Bihela (35) muha mkiristo mkazi wa Kijiji Cha kikoma kata ya Lusahunga wilaya ya Biharamulo ambapo gali Hilo lilikuwa likitokea Nyamalagala wilaya ya Biharamulo kuelekea benako wilaya ya ngara .
Sambamba na hayo marehe waliyo fariki katika ajali hiyo ni Nyawenda Bihela (35)   Dereva na mmiliki wa Toyota succeed,  Jesca Leonard (45), Magreth Sekanabo (14) Adidas Sekanabo (12),Zabron Sekanabo (6), Vestina Sekanabo (8) hawa wote ikiwa Ni kutoka familia moja , Michael Charles (28), na Majaliwa Kanundo (32)  ambao walikuwa wamefuatana na Dereva wa Gari Aina ya Toyota ambapo mpaka Sasa maiti zao zipo katika kituo Cha afya Cha Nyakanazi.
Mtuhumiwa Vicent Gakuba, Dereva  wa Gari namba RAF 129W Mercedes Benz alijaribu kutoroka Mara baada ya ajali hiyo lakini Jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata tarehe 11 July mwaka huu majira ya saa 10:00  huko katima kizuizi Cha kahaza Rusumo akiwa ndani ya Lori linaloelekea Rwanda akiwa katika harakati za kukwepa kukamatwa na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani Mara baada ya taratibu kukamili za kiupelelezi.

About the author

mzalendoeditor