Featured Michezo

TAMISEMI QUEENS YAICHAKAZA VIBAYA UDSM

Written by mzalendoeditor

Asila Twaha, Dar es Salaam

Timu ya Tamisemi Queens imeendelea kuwa tishio kwa kuonesha mabavu yake kwa kuichapa timu ya UDSM goli 65 -14 katika mpira wa netiboli.

Mechi hiyo iliyochezwa leo majira ya saa tatu asubuhi katika uwanja wa ndani uliopo uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ikiwa Tamisemi Queens inaendelea kuwanyoosha wapinzani wake tangu walipoanza mchezo huo.

TAMISEMI iliendelea kuicharaza UDSM na kushindwa kufurukuta huku wachezaji wa timu hiyo kubanwa na kukosa pa kuhemea kwa uwingi wa goli walizochapwa.

Wachezaji wa upande wa TAMISEMI GK- Mecklina Lucas, GD-Merisiana Kinzenga na WD Asha Rashid kuhakikisha kunakuwa na ulinzi mkali wa kutokupelekwa kwa goli katika lango la Tamisemi Queens.

Mpaka mchezo unafikia mapumnziko Tamisemi Queens ilikuwa inaongoza goli 33 na kwa upande wa UDSM ikiwa imepata goli 10.

Aidha, mpaka mpira unaisha Timu ya TAMISEMI Queens ilikuwa imeshinda goli 65 UDSM ikiwa imepata goli 14.

About the author

mzalendoeditor