KLABU ya Simba imendelea kushusha vifaa kila siku ikifika saa saba mchana mara baaada ya leo kutmbulisha mchezaji anayemudu kucheza nafasi ya benki/kiungo Mkabaji Nassoro Kapama kutoka Kagera Sugar.
Kapama anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na amekuwa mzawa wa pili mpya kusajiliwa Simba baada ya mshambuliaji Habib Kyombo kutoka Mbeya Kwanza iliyoshuka Daraja.
Wachezaji wengine ambao wamesajiliwa niĀ kiungo Mnigeria, Victor Akpan kutoka Coastal Union na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri kutoka Zanaco ya kwao.