Featured Kimataifa

WAZIRI MKUU JAPAN APIGWA RISASI WAKATI AKITOA HOTUBA

Written by mzalendoeditor

                                      Waziri Mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe

WAZIRI Mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe amepigwa risasi wakati akitoa hotuba katika hafla moja mjini Nara, Abe alipigwa risasi mara mbili, huku risasi ya pili ikimpiga mgongoni na kumfanya aanguke chini, ripoti zinasema kuwa alifanya tukio hilo amekamatwa.

Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii,  zinaonekana kuonyesha wahudumu wa afya wakiwa wamemzunguka Bw Abe katikati ya barabara kabla ya  kukimbizwa hospitalini.

Bw Abe, ambaye alikuwa Waziri Mkuu aliyekaa muda mrefu zaidi madarakani nchini Japan, alijiuzulu mwaka 2020 akitoa sababu za kiafya.

Chanzo:Global Tv

About the author

mzalendoeditor