Featured Kitaifa

TIC YATOA ELIMU YA UWEKEZAJI MAONESHO YA 46 YA SABASABA

Written by mzalendoeditor

 

 Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bi. Pendo Gondwe akiongea na waandishi wa Habari kwenye Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar-es-Salaam.
**

Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC)  kinawakaribisha wananchi na wadau wote wa Uwekezaji  kutembelea banda lao katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho hayo Meneja Uhusiano na Mawasiliano Bi. Pendo Gondwe amesema ” Kama ilivyo kauli mbiu ya mwaka huu katika maonyesho haya ya Sabasaba inayosema Tanzania mahali sahihi kwa Uwekezaji na Biashara  Kwa hakika ni mahala sahihi pa Uwekezaji hivyo tunakuomba wewe Mdau wa Uwekezaji uweze kufika katika mabanda yetu ili uweze kujifunza masuala mbalimbali ya Uwekezaji. 

Tunapatikana katika Banda namba 14 PTA na jengo la Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Majukumu ya TIC ni pamoja na; Kuhamasisha Uwekezaji, kuwahudumia wawekezaji kupitia kituo cha mahala pamoja, Kuratibu majukumu mbalimbali yahusuyo Uwekezaji na kuishauri Serikali juu ya kuboresha mazingira ya Uwekezaji na Uwekezaji kwa ujumla.”

 

Ili kupata taarifa zetu mbalimbali na maelekezo ya banda la TIC lilipo katika maonyesho ya sabasaba tafadhari tupigie kwa namba 0734 989471.

About the author

mzalendoeditor