RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakipata maelezo ya Bidhaa za Vifuu kutoka kwa Mwakilishi wa Kikundo cha Wajasiriamali cha Kiumbe Mzito kutoka Masingini Bi.Mwanaid Maneno, wakati akitembelea maonesho ya Wajasiriamali yalioandaliwa katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, Mama Mariam Mwinyi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, wakimsikiliza Mwakilishi wa Kikundi kutoka Burundi Bi. Chantal Birarondekwa, wakati akitembelea maonesho ya bidhaa za Wajasiriamali mbalimbali yaliyofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, Mama Mariam Mwinyi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said,na (kulia kwa Rais) Naibu Katibu Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Stephen Mlote, wakimsikiliza Mwakilishi wa Kikundi Nia Safi Women Group.Bi. Neema Batraham, wakati akitembelea maonesho ya bidhaa za Wajasiriamali mbalimbali yaliyofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani.(
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akijumuika na Wananchi wakati Kikundi cha Taarab cha Zanzibar One wakitowa burudani na kuimba wimbo maalum wa kumpongeza Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani, yaliyoadhimishwa katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja.
WAGENI Waalikwa na Wananchi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani ) akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani, yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi “B” Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani, yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja
BAADHI ya Viongozi wa Serikali na wageni waalikwa katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani wakipiga makofi kushangilia na kumpongeza Rais wa Zanzibar naMwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) wakati akihutubia katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi”B”Unguja leo 7-7-2022.(Picha na Ikulu)