Featured Kitaifa

DK.CHUWA ATAKA WATENDAJI NGAZI YA MKOA,WILAYA,KATA NA MITAA KUWA WAZALENDO ILI KUFANIKISHA ZOEZI LA SENSA

Written by mzalendoeditor

Na Eva Godwin-DODOMA

MTAKWIMU mkuu wa serikali Dkt Albina chuwa ametoa wito kwa watendaji ngazi ya mkoa,wilaya, kata,mitaa,kufuata sheria kuhakikisha wanafuata utaratibu uliowekwa pamoja na uzalendo mbele ili kufanikisha zoezi la sensa ya watu na makazi la kitaifa na kimataifa hapa nchini.

Ameyasema hayo July 6,2022 wakati akitoa taarifa yake kuhusu kuanza kwa mafunzo ya wakufunzi wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ngazi ya mkoa Jijini Dodoma

Dkt. Chuwa amesema kuwa lengo la mafunzo ya wakufunzi wa Sensa ya watu na Makazi ni kuwajengea uwezo na uelewa wa pamoja kuhusu nyenzo zote za sensa pamoja na utaratibu mzima.

“Fateni utaratibu uliowekwa pamoja na uzalendo uwe kipaumbele kama Nchi yetu ili zoezi la Sensa liende kama tulivyopanga najua viongozi wenu wapo watasimamia na kufuata kanuni za usimamizi”,amesema

“Lengo letu ni kuwajengea uwezo pamoja na uelewa juu ya Sensa ya Watu na Makazi la Kitaifa na Kimataifa Nchini”.Amesema Dk Chuwa

Aidha,Dkt Chuwa amesema mafunzo hayo washiriki watakaofaulu wajibu wao ni kwenda kufundisha wasimamizi na makarani wa sensa ngazi ya wilaya,taarafa,sheria kwa muda wa siku 21.

“Kuanzia tarehe 29 julai hadi Agost 18.2022 mafunzo ya sensa katika ngazi ya wilaya yataanza na tarehe 29 julai hadi Tarehe 18 Agost 2022 ni makarani,wasimamizi wa maudhui na wasimamizi wa Tehama”,amesema

“Na kuanzia Tarehe 6 hadi 26 julai 2022 kamati za sensa ngazi ya wilaya,kata,mitaa na sheria watakuwa na jukumu kubwa la kukamilisha mchakato wa ajira za makarani na wasimamizi wote nchi nzima na kuhakikisha kuwa makarani wote laki mbili na Elfu Tano(205,000)wanatoka katika maeneo wanayoishi”.Amesema Dkt.Chuwa

About the author

mzalendoeditor