Featured Kitaifa

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAPOKEA MAGARI KUMI KUTOKA UNDP

Written by mzalendoeditor

Na Mwandishi wetu DSM

Wizara ya Maliasili na Utalii imekabidhiwa  magari kumi kutoka  Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) kwa ajili ya kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya ujangili wa wanyamapori 

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa magari hayo,  Katibu Mkuu wa  Maliasili na Utalii , Prof. Eliamani Sedoyeka amesema Magari hayo yanakwenda kwenye kaya 10 tofauti tofauti kwa  lengo la kuhakikisha kuwa  rasilimali za wanyamapori  zinalindwa kikamilifu

“Nchi yetu ipo katika mapambano makali dhidi ya ujangili na  sisi kama wizara ya maliasili tuna jukumu la kuhakikisha  rasilimali zetu zinaendelea kutumikakwa ajili  ya kizazi cha sasa  na vizazi vijavyo” Amesema Prof. Sedoyeka 

 Amesisitiza kuwa katika jitihada za kupambana na ujangili,  Wizara imeendelea kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi ikiwemo  UNDP,    ” UNDP imetusaidia katika kuijengea  uwezo  timu yetu pamoja na kutuongezea vitendea kazi ambapo leo hii wametukabidhi magari 10 kwa ajili ya  mapambano hayo” 

Kutokana na jitihada hizo,  Prof. Sedoyeka amesema odadi ya wanyama  wakubwa kama vile  tembo ba faru  waliokuwa  wakipungua kutokana na tatizo la ujangili  wameanza kuongezeka kwa kasi

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania,  Christine Musisi amesema kumekuwa na ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kipindi cha muda mrefu na hivyo  wamekuwa wakivutiwa na juhudi zinazofanywa na Wizara hiyo katika mapambano dhidi ya  ujangili wa wanyamapori 

” Tumeendelea kushirikiana na Wizara kwa kuwapatia vitendea kazi, kuwajengea uwezo watumishi na kupitia jitihada hizo idadi ya wanyama kama vile tembo imeongezeka maradufu, alisema Mwakilishi wa UNDP, Musisi

Mwakilishi huyo wa UNDP amesisitiza kuwa UNDP  itaendelea kuwa mdau mkubwa  wa uhifadhi kwa kuhakikisha kuwa wanyamapori wa Tanzania  wanaendelea kuwa salama kwa ajili ya manufaa makubwa ta  jamii na uchumi wa nchi.

About the author

mzalendoeditor