Featured Kitaifa

ANNE MAKINDA AZINDUA SALUNI YA KISASA ‘BIG 5 BARBERSHOP & SAUNA’ MJINI SHINYANGA

Written by mzalendoeditor

Muonekano wa sehemu ya kunyolea nywele ndani ya Big 5 Barbershop & Sauna

Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda akiangalia vifaa vya kutolea huduma kwa watoto ndani ya  Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga . Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda akiwa ndani ya Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna iliyoboreshwa zaidi Mjini Shinyanga leo Julai 2,2022 baada ya kuizindua.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda amezindua Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna iliyoboreshwa zaidi Mjini Shinyanga huku akimpongeza mmiliki wa Saluni hiyo Adam Mwihechi kwa uwekezaji huo ambao umewezesha kupatikana kwa ajira 25 za vijana.
 
Makinda ambaye ni Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 ametoa pongezi hizo leo Jumamosi Julai 2,2022 akielekea kwenye Bonanza la Sensa ya Watu na Makazi 2022 lililoandaliwa na kundi la mtandao wa Kijamii maarufu SHY TOWN VIP Mjini Shinyanga.
 
“Nakupongeza kwa ubunifu huu, hii ni sehemu nzuri na haujasema siri uliyaona wapi haya mambo mazuri ukaamua kuyaleta hapa, ni saluni ya kisasa ambayo kila mtu lazima afurahie huduma, nimeona wafanyakazi wana furaha. Wengi wetu tutakuja kupata huduma hapa kwani kuna huduma nzuri na panafurahisha sana”.
 
“Nakushukuru kwa kuajiri vijana 25 kwani umeleta ajira kwa vijana hawa. Naomba vijana mfanye kazi kwa bidii, kushirikiana na kujituma”,amesema Makinda.
 
Makinda ametumia fursa hiyo kumshauri mmiliki wa Saluni hiyo ya kisasa kutumia mitandao ya kijamii kutangaza huduma anazotoa huku akiishukuru Benki ya NMB kwa kumpatia mkopo mmiliki wa Saluni hiyo.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi na Mmiliki wa Big 5 Barbershop & Sauna bw. Adam Mwihechi amemshukuru Mhe. Anne Makinda kwa kuzindua saluni ya kisasa ‘iliyoboreshwa zaidi’ akisema sasa ina viwango vya kimataifa.
 
Amezitaja huduma wanazotoa kuwa ni huduma zote za saluni ambapo sasa wana sehemu maalumu ya kuhudumia watoto, na chumba maalumu kwa kuhudumia mtu mmoja “VIP” na huduma zingine kede kede ikiwemo Barbershop, kuosha miguu, Gym, Game Centre, Sauna, Massage na muziki.
 
“Tunawashukuru sana Benki ya NMB wameendelea kutushika mkono kwa kutupatia mkopo na sasa tunaendelea kupanua huduma na kuzifanya kuwa za kisasa zaidi”,amesema Mwihechi.
 
Naye Afisa Mahusiano wa Benki ya NMB tawi la Manonga, William Tumbo amesema benki hiyo imekuwa ikitoa ushirikiano kwa Big 5 Barbershop & Sauna kwa kuipatia mikopo yenye riba nafuu tangu mwaka 2013 huku akiwasihi wananchi kuchangamkia fursa zinazotolewa na benki hiyo.
 
Big 5 Barbershop & Sauna ipo pembezoni mwa barabara ya Mwanza – Shinyanga jirani na Jengo la NSSF Mjini Shinyanga. Wasiliana nao kwa simu namba 0767446337
 
Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda akikata utepe kuzindua Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga leo Julai 2,2022. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude, kulia ni Mwenyekiti wa SHY TOWN VIP, Mussa Ngangala. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda akizindua Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga leo Julai 2,2022. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude, kulia ni Mwenyekiti wa SHY TOWN VIP, Mussa Ngangala. 
Mwenyekiti wa SHY TOWN VIP, Mussa Ngangala akizungumza wakati Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda (kulia) akizindua Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna iliyoboreshwa zaidi Mjini Shinyanga leo Julai 2,2022. 
Mkurugenzi wa Big 5 Barbershop & Sauna, Adam Mwihechi (kushoto) akizungumza wakati Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda akizindua Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna iliyoboreshwa zaidi Mjini Shinyanga leo Julai 2,2022. 
Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda akiwa ndani ya Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna iliyoboreshwa zaidi Mjini Shinyanga leo Julai 2,2022 baada ya kuizindua.
Wafanyakazi wa Big 5 Barbershop & Sauna wakifuatilia matukio wakati Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda akizindua Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga leo Julai 2,2022. 
Mkurugenzi wa Big 5 Barbershop & Sauna, Adam Mwihechi (kushoto) akimuonesha Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda vifaa mbalimbali vya kutolea huduma ndani ya  Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga 
Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda akiwa amekaa kwenye kiti ndani ya Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga 
Mkurugenzi wa Big 5 Barbershop & Sauna, Adam Mwihechi (kushoto) akimuonesha Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda vifaa mbalimbali vya kutolea huduma ndani ya  Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga 
Mkurugenzi wa Big 5 Barbershop & Sauna, Adam Mwihechi (kushoto) akimuonesha Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda vifaa mbalimbali vya kutolea huduma ndani ya  Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga 
Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda vifaa vya kutolea huduma kwa watoto ndani ya  Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga 
Mkurugenzi wa Big 5 Barbershop & Sauna, Adam Mwihechi (kushoto) akimuonesha Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda vifaa mbalimbali vya kutolea huduma ndani ya  Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga 
Mkurugenzi wa Big 5 Barbershop & Sauna, Adam Mwihechi (kushoto) akimuonesha Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda vifaa mbalimbali vya kutolea huduma ndani ya  Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga 
Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda  akiwa ndani ya  Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga 
 Afisa Mahusiano wa Benki ya NMB tawi la Manonga, William Tumbo  akizungumza wakati wa uzinduzi wa Big 5 Barbershop & Sauna
Mkurugenzi wa Big 5 Barbershop & Sauna, Adam Mwihechi (kulia) akifurahia jambo na Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda ndani ya  Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga 
Mkurugenzi wa Big 5 Barbershop & Sauna, Adam Mwihechi (kushoto) na Mwenyekiti wa Shy Town VIP, Mussa Ngangala wakipiga picha ya kumbukumbu na Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda ndani ya  Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga 
Wafanyakazi wa Big 5 Barbershop & Sauna wakipiga picha ya kumbukumbu na Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda ndani ya  Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga 
Wafanyakazi wa Big 5 Barbershop & Sauna wakipiga picha ya kumbukumbu na Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda ndani ya  Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga 
Wanachama wa SHY TOWN VIP , Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Joseph Mkude wakipiga picha ya kumbukumbu na Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda ndani ya  Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga 
Mkurugenzi wa Big 5 Barbershop & Sauna, Adam Mwihechi (wa pili kulia) akiagana na Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda baada ya kuzindua Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga
Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Mwenyekiti wa SHY TOWN VIP, Mussa Ngangala alipowasili kwa ajili ya kuzindua Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga. Kushoto ni Mkurugenzi wa Big 5 Barbershop & Sauna, Adam Mwihechi
Wafanyakazi wa  Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna  wakimsubiri Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda kwa ajili ya kuzindua saluni hiyo.
Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda akisalimiana na wafanyakazi wa Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga.
Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Anne Makinda akisalimiana na wafanyakazi wa Saluni ya Kisasa maarufu Big 5 Barbershop & Sauna Mjini Shinyanga.
 
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde  1 blog
 
About the author

mzalendoeditor