Featured Kitaifa

WAZIRI AWESO AZITAKA BODI ZA MAMLAKA ZA MAJI KWENDA KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAJI

Written by mzalendoeditor
WAZIRI wa maji Jumaa Aweso akifungua mafunzo  ya bodi na mejimenti za mamlaka za maji na usafi wa mazingira nchini yanayoendelea mkoani Arusha.
katibu mkuu wa wizara ya maji Mhandisi Anthony Sanga akiongea katika mafunzo ya bodi na mejimenti za mamlaka za maji na usafi wa mazingira nchini mkoani Arusha
Mwenyekiti wa bodi ya maji ya mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Arusha(AUWSA) Enjinia Richard Masika akitoa neno la shukurani baada ya waziri wa maji Jumaa Aweso kufunga mafunzo ya bodi na mejimenti za mamlaka za maji na usafi wa mazingira nchini.
Mkurugenzi wa mamlaka za maji mijini,CPA Joyce Msilu akiongea katika mafunzo ya bodi na mejimenti za mamlaka za maji na usafi wa mazingira nchini.
Baadhi ya wajumbe wa bodi na mejimenti za mamlaka za maji na usafi wa mazingira nchini wakiwa katika mafunzo yanayoendelea mkoani Arusha.
…………………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Waziri wa maji Jumaa Aweso amewataka bodi za mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira kwenda kupunguza upotevu wa maji  kwani sio jambo jema kuona maji yakimwagika njiani ilhali wananchi hawana maji 

Waziri Aweso aliyasema hayo  leo June 29, 2022 wakati akifungua mafunzo ya bodi na mejimenti za mamlaka za maji na usafi wa mazingira nchini yanayoendelea mkoani Arusha ambapo alisema kuwa serikali imetumia fedha nyingi ku wekeza miradi ya maji hivyo wakasimamie maji hayo yasipotee bali yawafikie wananchi ili wapate huduma ya maji safi na salama.
Alisema kuwa maji yana umuhimu wa kipekee ambapo kutokana na upatikanaji wa maji  asilimia 50 ya magonjwa yanayoambukiza yanapungua, wanajisikia vibaya kuona wizara yao inakuwa wizara ya kero na lawama lakini hivi Sasa Imani iliyopo ni kubwa kwani wanafanya kazi kubwa lakini isiwe ni nguvu ya soda.
“Tumepewa mamlaka ya kuteua bodi za maji ili zitusaidie majukumu katika maeneo waliyopangiwa mambo yaende vizuri kwani kazi tunayoifanya sio kwamba ni huduma tuu lakini pia ni sawabu, kumpelekea mtu maji Ile dua anayoitoa inatoka moyoni hivyo tukafanye kazi ili Yale malengo tuliyojiwekea kufika 2025 maji yaweze kupatikana vijijini kwa asilimia 85 na mijini kwa asilimia 95 tuweze kuyafikia,”Alisema Aweso.
“Kazi mahusisu za bodi ni kusimamia taasisi na hamuwezi kufanya mapinduzi wala malengo tunayoyataka kama bodi hazitakuwa na umoja na mshikamano mkawe pamoja mjue majukumu ya bodi na sio bodi zikawe hohehahe, vitu viende kwa utaratibu ili mambo yaende vizuri,” Alisisitiza.
Aliwataka kwenda kuonyesha matokeo chanya kutokana na mafunzo waliyoyapata ikiwemo kushughulikia malalamiko ya wateja na watumishi kwa wakati pamoja kuajiri watumishi wenye sifa stahiki, watakaongeza tija kwa mamlaka ikiwa ni pamoja na kutengeneza mahusiano na mashirikiano na taasisi nyingine ikiwemo TARURA ili kuondoa mivutano isiyo na tija.
Kwa upande wake katibu mkuu wa wizara ya maji mhandisi Antony Sanga alisisitiza  wajumbe wa bodi kuziekewa mamlaka za maji kwa kukaa na watumishi kujua changamoto,kero na malalamiko  yanayowakabili na kuzitafutia ufumbuzi lakini kufahamu kazi zinazotekelezwa na mamlaka kwa kutembelea na kukagua miradi inayoendea ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua stahiki ya kutatua changamoto zinazotolewa katika mamlaka.
Alifafanua kuwa wizara inapitia mapinduzi makubwa tumetoka  kuwa wizara ya lawama hadi kuwa wizara ya utatuzi ambapo bado changamoto za maji zipo lakini matumaini ya kuwapatia wananchi maji ni makubwa kwani huduma za maji zimeboreka na kuna miradi ambayo imekamilika na inafanya kazi pamoja na mingine ambayo inaendelea kutekelezwa.
Naye Mkurugenzi wa mamlaka za maji mijini,CPA Joyce Msilu alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa wa masuala mbalimbali yanayotoa dira ya utekelezaji wa mjukumu ya bodi ya wakurigenzi na manejimenti katika kuzimamia na kuziendesha mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira ili wananchi waweze kupata huduma bora.
Mwenyekiti wa bodi ya maji ya mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Arusha(AUWSA) Enjinia Richard Masika akiongea kwa niaba ya bodi zingine alisema kuwa watazingatia na kutenda kwa ufanisi maagizo yote waliyopewa ili kuweza kufikiaalengo na kuleta ufanisi na tija katika usambazaji wa maji, usafi wa mazingira na ukusanyaji wa mapato.

About the author

mzalendoeditor