Featured Kitaifa

TANZANIA NA ZAMBIA KUENDELEZA USHIRIKIANO SEKTA YA MADINI

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Madini na Maendeleo ya Migodi wa Zambia, Paul Kabuswe,akisalimiana na Viongozi wa Wizara ya Madini mara baada ya kuwasili nchini akiwa na ujumbe kutoka Zambia ukiongozwa na  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na wataalam wengine wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ya kujifunza kuhusu usimamizi wa sekta ya madini hususani kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zinazofanywa na wachimbaji wadogo leo Juni 29,2022 jijini Dodoma.

Ujumbe kutoka Zambia ukiongozwa na  Katibu Mkuu wa Wizara wa Wizara ya Madini na Maendeleo ya Migodi  na wataalam wengine wakifatilia majadiliano mbalimbali kutoka Wizara ya Madini  wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ya kujifunza kuhusu usimamizi wa sekta ya madini hususani kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zinazofanywa na wachimbaji wadogo leo Juni 29,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko,akiteta na Waziri wa Madini na Maendeleo ya Migodi wa Zambia, Paul Kabuswe,ambaye yupo nchini na ujumbe kutoka Zambia ukiongozwa na  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na wataalam wengine wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kujifunza kuhusu usimamizi wa sekta ya madini hususani kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zinazofanywa na wachimbaji wadogo.

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumpokea Waziri wa Madini na Maendeleo ya Migodi wa Zambia, Paul Kabuswe,ambaye  yupo nchini  kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ya kujifunza kuhusu usimamizi wa sekta ya madini hususani kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zinazofanywa na wachimbaji wadogo.

 Waziri wa Madini na Maendeleo ya Migodi wa Zambia, Paul Kabuswe,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini  kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ya kujifunza kuhusu usimamizi wa sekta ya madini hususani kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zinazofanywa na wachimbaji wadogo.

……………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Madini na Maendeleo ya Migodi wa Zambia, Paul Kabuswe,amesema kwa usimamizi mzuri wa mfumo  uliopo kwenye sekta ya madini nchini umewafanya kuja kujifunza namna wanavyosimamia sekta hiyo ili kunufaisha wananchi wao.

Waziri Kabuswe ameyasema leo Juni 29,2022 jijini Dodoma mara baada ya kuwasili nchini akiwa na ujumbe kutoka Zambia ukiongozwa na  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na wataalam wengine wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kujifunza kuhusu usimamizi wa sekta ya madini hususani kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zinazofanywa na wachimbaji wadogo.

Waziri Kabuswe amesema nchi hizo mbili zimekuwa na uhusiano na ushirikiano wa kipindi kirefu na nchi hiyo imeshuhudia namna uchimbaji mdogo wa madini nchini ulivyofanikiwa hivyo, ujumbe huo umefika kujifunza na kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kusimamia sekta ya madini.

“Sisi ni serikali mpya tupo kwenye ofisi kwa takribani miezi 10 kwa hiyo tumeona tuje kujifunza kwa kuwa miongoni mwa vitu ambavyo Tanzania imefanya vyema ni usimamizi wa rasilimali za madini wachimbaji wadogo,”amesema Waziri Kabuswe

Amesema kuwa wamekuja kujifunza namna watakavyosimamia sekta ya madini ya Zambia  ili kuwanufaisha wananchi wake.
 
‘‘Tumeona hatunufaiki ipasavyo na sekta ya madini, tunataka watu wetu wapate ajira kwenye nafasi muhimu kupitia sekta hii, tunataka wananchi wanufaike ipasavyo ili vizazi vyetu vijavyo visikute mashimo tu, tunayo madini kama dhahabu, shaba, manganese tunataka madini haya yalete tija kwa sababu tumeona namna Tanzania inavyofanya vizuri sana tumeona ipo haja ya sisi kujifunza na kubadilishana uzoefu,’’ amesema Waziri Kabuswe.
 
Aidha Waziri Kabuswe ameleeza kuwa, ipo haja kwa wizara yake kuwaleta tena wataalam wake kuja kujifunza kwa kina.

Kwa upande wake Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko,amesema kuwa kiongozi huyo na ujumbe wake wapo nchini kujifunza usimamizi wa sekta ya madini hasa uchimbaji wa dhahabu na uchimbaji mdogo.

Dkt.Biteko amesema kuwa nchi ya Zambia inatarajia kufanya marekebisho ya Sera na Sheria zake za madini hivyo ujumbe huo umefika kujifunza namna wachimbaji wadogo wanavyofanya shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu, namna biashara ya madini ya dhahabu inavyofanyika kupitia masoko ya madini jambo ambalo limefanya mfumo wake kuwa mkubwa na mfano kwa nchi nyingine Afrika na duniani.

‘Waziri Kabuswe atakwenda kwenye machimbo kuangalia wanavyochimba wachimbaji wadogo na kutembelea masoko ya madini yaliyopo nchini’amesema Dkt.Biteko

About the author

mzalendoeditor