Featured Michezo

MPOLE AMKIMBIZA MAYELE ,ATWAA KIATU CHA UFUNGAJI BORA WA LIGI KUU YA NBC 2021/22

Written by mzalendoeditor
MSHAMBULIAJI Mzawa, George Mpole ndiye mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kufunga bao la 17 leo, Geita Gold ikilazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Mpole amempiku mshambuliaji Mkongo wa Yanga, Fiston Kalala Mayele aliyemaliza na mabao 16 baada ya leo kushindwa kufunga kwa mara ya pili mfululizo timu yake ikiibuka na ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar.
Msimu wa Ligi Kuu 2021-2022 umehitimishwa leo, timu za Mbeya Kwanza na Biashara United zikishuka daraja, huku Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons zikienda katika mechi za mbili za mchujo baina yao nyumbani na ugenini kuwania kubaki Ligi Kuu.
Timu itakayoshinda itabaki Ligi Kuu na itakayofungwa itakwenda kumenyana na JKT Tanzania kutoka Championship na mshindi ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.

About the author

mzalendoeditor