Featured Kitaifa

SEKTA ZA MAJI  SMT NA SMZ ZAKUTANA KUJADILI  MIKAKATI YA MASHIRIKIANO 

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Maji (SMT) Mhe.Jumaa Aweso,akizungumza wakati wa kikao cha Wizara ya Maji, Nishati Na Madini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) chenye lengo la kuweka mikakati ya mashirikiano kilichofanyika leo Juni 27,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Maji,Nishati na Madini (SMZ) Shaib Hassan Kaduara,akizungumza wakati wa kikao cha Wizara ya Maji (SMT) chenye lengo la kuweka mikakati ya mashirikiano kilichofanyika leo Juni 27,2022 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Maji.Mhandisi Maryprisca Mahundi,akizungumza wakati wa kikao hicho.

Waziri wa Maji (SMT) Mhe.Jumaa Aweso,akiwa na Waziri wa Maji,Nishati na Madini (SMZ) Shaib Hassan Kaduara katika picha ya pamoja mara baada ya kikao cha pamoja chenye lengo la kuweka mikakati ya mashirikiano kilichofanyika leo Juni 27,2022 jijini Dodoma.

……………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

SEKTA za Wizara ya Maji za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Wizara ya Maji, Nishati Na Madini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia Mawaziri wake wamekutana kuweka mikakati ya mashirikiano yenye lengo la kuhakikisha watanzania kwa ujumla wanapata huduma bora ya maji.

Akifungua Kikao hicho leo Juni 27,2022 jijini Dodoma Waziri wa Maji (SMT) Mhe.Jumaa Aweso,amesema kuwa wote kwa pamoja wana jukumu kubwa la kuhakikisha huduma hiyo muhimu inapatikana kwa watanzania wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Serikali itahakikisha haitakuwa kikwazo katika kuwapatia huduma bora ya maji wananchi wa kutoka upande wa Bara na upande wa Zanzibar.”amesema Aweso

“Kikao hiki cha mashirikiano baina ya Wizara ya Maji Nishati na Madini (SMZ) na Wizara  ya maji (SMT) ,ni kwa ajili ya kujengeana uwezo na kupeana ushirikiano katika kuleta mageuzi makubwa katika wizara zetu za maji.”amesema Aweso

Waziri Aweso amesema kuwa kwa upande wa Tanzania Bara ,Wizara yake imefanya jitihada kubwa ya kuhakikisha inapunguza changamoto zilizokuwa zikiikabili wizara hiyo ambayo ilionekana kero kwa wananchi.

Aidha Aweso amewaasa watendaji wa pande zote mbili za Muungano kutekeleza wajibu wao kwa uadilifu katika kuwatumikia watanzania n kuhakikisha wanapata huduma hiyo muhimu.

Kwa upande wake Waziri wa Maji,Nishati na Madini (SMZ) Shaib Hassan Kaduara amesema kuwa ushirikiano wa Bara na Zanzibar unakwenda kutatua changamoto ya maji Zanzibar.

Waziri Kaduara amesema kuwa  katika ziara hiyo,wataalam kutoka Zanzibar wanachukua utaalam uliotumika Bara ambao umeaidia kutatua changamoto ya maji licha ya kuwa upande huo una wananchi wengi.

Aidha amesema kwa licha ya kuwa wana visima vya maji 371 vinavyotumia umeme lakini bado wana changamoto ya maji kutokana na uzalishaji kupungua kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto hiyo wanaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji ikiwemo mradi wa Wana mkopo wa Serikali ya India wa milioni 198.2 ambapo wanajenga tenki lenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 32.

‘Mradi huo utakapokamilika itaondoa changamoto ya maji kwa maeneo ya mjini kwa asilimia 90.’amesema

About the author

mzalendoeditor