Featured Kitaifa

RC MALIMA ASISITIZA VIWANGO BARABARA ZA TANGA

Written by mzalendoeditor

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amemhimiza mkandarasi
anayesimamia ujenzi wa Barabara ya Tanga-Pangani kwa kiwango cha lami
yenye urefu wa Km 50, kuzingatia viwango vyote vya ubora katika
kukamilisha barabara hiyo ili iendane na fedha za Watanzania
zilizotolewa kwa ajili hiyo.
Amesema
barabara hiyo ni muhimu kwenye mfumo wa barabara za kitaifa na
kimataifa si tu kwa ajili ya Tanga, kwani inaenda kuunganisha na Kenya.

Malima
alisema hayo wakati akikagua barabara hiyo na nyingine za mkoa huo
zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) na Wakala wa
Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura).

“Kimsingi
barabara hii inapunguza zaidi ya Km 120, inafupisha mtandao mzima wa
kwenda hadi Mombasa (Kenya) kwa sababu matarajio ni babarabara hii
kuingia hadi kwenye mtandao wa Afrika Mashariki.
“Kwa
hiyo kukamilika kwa barabara hii ni muhimu sana lakini kwa bahati mbaya
barabara hii imechelewa kwa sababu mbalimbali kwani ilikuwa Km hizo 50
ilikuwa zimalizike  Novemba mwaka jana lakini hapo katikati ikaingia
corona, matatizo ya fidia kwa upande wa Tanga na migogoro mingine kwa
hiyo ikachelewa ikapelekwa hadi Desemba mwaka huu,” alisema Malima.
Aidha,
aliongeza kuwa bado inaonekana kwa asilimia zilizofikiwa maeneo ya lami
yanaweza kufikiwa kama Km 30 hadi kufikia Desemba lakini kwa sasa
tunaona kasi inakwenda vizuri zaidi kuliko ilivyokuwa kabla.
“Kwa
hiyo niishukuru serikali kwani miezi kama sita iliyopita tulikuja
kukagua na Waziri Mbarawa (Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi – Profesa Makame
Mbarawa) tuliweka mkataba usio na maandishi baina ya serikali, Mkoa wa
Tanga na wizara kwamba na sisi tutakuwa na utaratibu wa kupita na
kukagua maendeleo ya pamoja na wahandisi wa mkoa, Tanroads, Kamati ya
Usalama ya Mkoa na pale ambapo tunaona kuna ucheleweshaji wa jambo moja
au jingine basi tutatumia fursa hiyo kumwambia waziri kwamba jamani kule
barabara yetu mliyotuachia tufanye uangalizi na usimamizi kuna haya na
haya.
“Hatua hii inatusaidia
kujadili barabara ambazo tumeziona kwa macho katika Kikao cha Bodi ya
Barabara na wakati tunapokea taarifa ya Tanroads na Tarura mkoa tunakuwa
na uelewa wa barabara hizo kwa hiyo wakisema pale daraja sijui
limefanya nini tunasema hapana tumeiona.
“Kwa
mfano kama sasa msimamizi anakwamishwa kwa sababu kuna fedha
zimechelewa kidogo kama bilioni tisa hivi ambazo zinamuweka kwenye hali
ya kuchelewesha kazi na kupata kisingizio. Kwa hiyo changamoto zilizopo
hapa tumeziona na tumepata taarifa kutoka kwa wahandisi,” alisema
Malima.
Kwa
upande wake Meneja wa Tanroads Mkoa wa Tanga, Mhandisi Eliazary
Rweikiza alisema mradi huo unaosimamiwa na Mkandarasi Kampuni ya China
Henan International Cooperation Group Ltd. ya nchini China kwa gharama
ya Sh bilioni 67.47 imefikia asilimia 37.6 ya utekelezaji na makubaliano
na mkandarasi ni kwamba ikamilike Desemba 5, mwaka huu.
Alibainisha
kuwa kuchelewa kukamilika kwa mradi huo kulitokana na changamoto
mbalimbali ikiwamo malipo kwani hadi kufikia Mei mwaka huu mkandarasi
alikuwa anaidai serikali Sh bilioni 9.64.
“Aidha,
changamoto za kuchelewa kulipa fidia kwa waliofuatwa na barabara ili
kupisha mradi, matakwa ya fidia kutoka kwa wamiliki wa maeneo hayo,
mkandarasi kuchelewa kulipwa malipo kwa wakati na upatikanaji wa maeneo
mazuri ya changarawe na ugonjwa wa corona ambao ulisababisha wataalamu
wa mkandarasi kuchelewa kuwasili eneo la kazi.

“Lakini
pia mwanzoni mwa mradi mkandarasi alikuwa na meneja wa mradi ambaye
alikuwa hajui Kiswahili wala Kiingereza na kusababisha mawasiliano ya
kiutendaji kuwa magumu. Changamoto hii kwa sasa haipo kwa kuwa meneja
huyo aliondolewa na kuletwa mwingine ambaye anajua Kiingereza na ana
,ipango mizuri ya kazi,” alisema

About the author

mzalendoeditor