Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATOA WITO KWA JAMII KUHUDUMIA WATOTO

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa pamoja na Baadhi ya Wake wa Viongozi mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Mfuko huo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Mfuko huo 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kazi mbalimbali za kijasiriamali zinazofanywa na wanufaika wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) katika maadhimisho ya kilele cha Mfuko huo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC  Jijini Dar es Salaam 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika kilele cha Sherehe ya miaka 25 ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo kwa Baadhi ya Wafadhili waliojitolea kuunga mkono  Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) katika maadhimisho ya kilele cha Mfuko huo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC  Jijini Dar es Salaam

Viongozi mbalimbali pamoja na Wanufaika wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Mfuko huo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyekiti wa EOTF Mama Anna Mkapa katika picha ya pamoja na Wake wa Viongozi mara baada ya maadhimisho ya miaka 25 ya Mfuko huo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Convention Center Jijini Dar es Salaam 

……………………………..

Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi kuacha kutelekeza Watoto kwa kuwa tabia hiyo inazalisha taifa lenye wananchi wasio madhubuti. 

Rais Samia ametoa wito huo leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Miaka 25 (Silver Jubilee) ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) katika ukumbi wa JNICC.

Aidha, Rais Samia ametoa wito kwa wazazi na Watanzania kuiunga mkono Serikali katika kutoa huduma kwa Watoto yatima. 

Rais Samia amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na Taasisi za kidini kutoa huduma pamoja na kuchangia maendeleo ya jamii hasa kwa wananchi wanaoishi katika mazingira duni. 

Kwa upande mwingine Rais Samia ameeleza kuwa Filamu ya The Royal Tour imesaidia kutoa fursa za kibiashara kwa wanawake wajasiriamali na hivyo kuwawezesha kujiinua kiuchumi.

Vile vile, Rais Samia amewataka wanawake wajasiriamali kutumia fursa hiyo kuzalisha bidhaa bora zaidi ili waweze kujiletea maendeleo na kujiinua kiuchumi.

Hali kadhalika, Rais Samia ametoa wito kwa EOTF kuendelea kuwajengea wanawake uwezo wa elimu ya biashara kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili waweze kuuza bidhaa nje ya nchi.

About the author

mzalendoeditor